Ebbeh – supu ya mihogo, samaki na ukwaju

Ebbeh ni supu ya mihogo inayokuwa pamoja na vyakula kama samaki na vingine toka baharini. Ni supu maarufu sana kwenye nchi za afrika magharibi. Ni nzuri kuinywa asubuhi au muda wowote kabla ya mlo kamili maana inaleta hamu ya kula kutokana na uwepo wa ukwaju, limao na pilipili.

Mahitaji

 • Mihogo kilo 1, menya na kata vipande vidogo vidogo
 • Samaki aliyekaushwa, gramu 200, toa miba na mifupa.
 • Kamba (prawns) gramu 200, menya maganda
 • Palm oil 400ml
 • Pilipili 2
 • Limao ½
 • Ukwaju 50g
 • Maji lita 3
 • Cubes 2
 • Chumvi  kijiko 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 Unaweza kutumia mchanganyiko wa samaki wa aina tofauti kwenye kuandaa hiki chakula.

 • Kwenye sufuria, chemsha mihogo na chumvi hadi ilainike.
 • Mihogo ikiiva, toa mihogo weka kwenye kinu au chombo cha kusagia chakula. Usimwage maji ya muhogo, hifadhi vizuri maana yatatumika kupikia.
 • Ponda mihogo kwenye kinu, au chombo cha kusagia, ili iwe laini. Rudishia mihogo kwenye maji yake, weka kwenye moto kisha weka viungo vyote vilivyobaki. Koroga pamoja, funika na acha vichemke pamoja.
 • Acha vichemke pamoja hadi supu iive vizuri. Unaweza kuongeza viungo kutokana na upendeleo wako – weka limao kwa unavyopendelea.
 • Supu ikishaiva, tenga na kula ikiwa bado ya moto.
 • Hii supu inaweza kuliwa na chakula kikuu au inaweza kuliwa kwa mkate, chapati na vitu vingine.

ebbeh-misosi-main-poor

 


MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi zenye iliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.