Garlic chicken

Kuku wa kuunga kwa viungo tofauti. Ladha bora na utamu wa kipekee. Ukitaka kujaribu mapishi tofauti ya kuku, jaribu kuku huyu uone raha yake.

Mahitaji

 • Kuku 1
 • Vitunguu saumu 6 au vijiko 15 vya chakula
 • Olive oil kikombe 1
 • Thyme kijiko 1 cha chai
 • Chumvi kijiko 1 cha chakula
 • Bay leaf 1
 • Rosemary kijiko 1 cha chai
 • Oregano kijiko 1 cha chai
 • Parsley kijiko 1 cha chai
 • Pilipili manga vijiko 2 vya chakula
 • Tangawizi kijiko 1 cha chai
 • Vinegar ya kutosha
 • Butter vijiko 3 vya chai
 • Vitunguu maji 2
 • Oyster sauce kijiko 1 na nusu cha chakula
 • Cornstarch kijiko 1 cha chakula
 • Mdalasini kijiko 1 cha chakula
 • Pilipili mbuzi 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Safisha kuku vizuri. Kata vipande vya kawaida kisha mpake chumvi. Hifadhi kwenye chombo pembeni.
 • Kwenye blender: Weka olive oil na viungo vyote - vitunguu saumu, thyme, bay, rosemary, oregano, parsley, tangawizi, vinegar, pilipili manga, kitunguu maji na oyster sauce. Saga kwa pamoja hadi viwe laini na uji uwe mzito. Toa na weka kwenye chombo pembeni.
 • Kata kuku vipande vidogo ili kurahisisha viungo kuingia vizuri kwenye nyama.
 • Mwaga mchanganyiko wa viungo kwenye bakuli lenye vipande vya kuku. Changanya vizuri sana hadi vipande vya kuku vilowe.
 • Toa vipande vya kuku, weka kwenye mfuko wa nylon, akiwa na rojo ya viungo, kisha funga mfuko vizuri na hifadhi kwenye jokofu kwa muda wa usiku kucha.
 • Ukiwa tayari kumuandaa , toa mfuko. Nyunyizia pilipili manga na paka unga wa cornstarch juu ya vipande vya nyama.
 • Pasha oven nyuzi joto 420°F (215°C).
 • Kwenye bakuli la kuokea kwenye oven, weka foil paper kisha paka butter juu yake.
 • Panga vipande vya kuku vizuri kwenye bakuli.
 • Weka bakuli kwenye oven, tega muda wa dakika 45. Chungulia mara kwa mara kuona kama wanaungua na ugeuze.
 • Jirambe na chakula murua cha Garlic chicken.

MAPISHI YAPENDWAYO

Creamy garlic potato
dakika 40
Walaji: 1

Chicken curry
dakika 30
Walaji: 5

Butter chicken
dakika 45
Walaji: 4

Garlic chicken
dakika 60
Walaji: 4

Toa maoni yakoalma
11:46, Mon 12 Jan 2015
Habari.nimevutiwa sana na blog yako kwani unapika vitu vizuri na rahisi kupatikana...although hii garlic chicken naona kama imekuwa na vitu vngi...naomba nifahamishe,thyme ni nn?nd hapo mwishoni ndo unaweka ule unga,did you mean the cornstarch?...otherwise,keep up the good work...all the best
Dadia Msindai
01:36, Tue 13 Jan 2015
Habari @alma, Karibu kwenye tovuti yetu ya misosi na asante kwa feedback yako.

Kuhusu Thyme, ni majani yanayotumika kama viungo. Nimejaribu kutafuta jina lake kiswahili ila nimekosa. Unaweza kuangalia picha kama hii yanavyoonekana.

Ni kweli, unga unaoweka ni cornstarch kwenye hatua za mwisho. Nimerekebisha ili iweze kuwa sahihi.

Kuhusu uwingi wa viambato, haya ndio mahitaji ya vitu vinavyotengeneza chicken garlic nzuri. Kama utakuwa na mapishi tofauti unaweza pia kutushauri, tunafurahi sana na feedback yako.

Asante kwa kutembelea misosi. Karibu tena.
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.