Grilled salmon

Mahitaji

 • Samaki nusu kilo
 • vitunguu saumu vilivyosagwa kijiko 1 na nusu
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chakula
 • Ndimu 1
 • Olive oil vijiko 6 vya chakula
 • Chumvi
 • Soy sauce vikombe 3
 • Lemon zest vijiko 3
 • Tangawizi kijiko 1
 • Mustard vijiko 2 vya chai
 • Maji

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chukua samaki, mtengeneze na msafishe vizuri. Muekee ndimu, pilipili manga, vitunguu saumu, chumvi, tangawizi na mustard kisha muweke kando.
 • Chukua bakuli kubwa, weka soy sauce, olive oil, lemon zest na maji. Changanya vizuri.
 • Chukua samaki, mweke kwenye mfuko wa nylon kisha weka viungo vyenye soy sauce.
 • Weka kwenye jokofu kwa masaa 2 kisha mtoe.
 • Washa moto, weka chuma cha kuchomea kikipata moto kipake mafuta.
 • Panga samaki, pika kila upande kwa dakika 6 huku ukiendelea kumpaka viungo vilivyobaki.
 • Pika na uhakikishe kama ameiva. Jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Macaroni matamu yenye njegere
dakika 15
Walaji: 2

Ndizi mshale za nazi
dakika 30
Walaji: 4

Cutlets za pilipili
dakika 5
Walaji: 4

Wali wenye nazi na maziwa
dakika 20
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.