Grilled Tandoori Chicken Sauce

Kuku anaweza kupikwa kwa mapishi tofauti na akawa mtamu. Haya ni mojawapo ya mapishi matamu ya kuku yanayojumuisha kuku wa kuoka na sauce yenye vionjo vitamu vya viungo. Utamu wa nyama ya kuku ukichanganya na sauce yenye mchuzi mzito wa nyanya kinachopatina ni zaidi ya mboga, bali ni ladha tamu ya kuifanya siku yako kupendeza.

Mahitaji

Kwa ajili ya kuoka kuku

 • Kuku vipande 4
 • Tandoori sauce
 • Tangawizi ya unga kijiko 1 kidogo
 •  Kitunguu saumu 1
 • Chumvi
 • Limao au ndimu 1, au pia unaweza kutumia vinegar

Kwa ajili ya sauce

 • Mafuta ya kula, nimetumia mafuta ya zaituni (Olive oil)
 • Pilipili manga
 • Limao
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Chumvi
 • Karoti 2
 • Bamia 4
 • Kitunguu maji kikubwa 1
 • Cayenne pepper 2
 • Nyanya 2 kubwa
 • Nyanya ya kopo vijiko 3 vikubwa (Kuongeza ladha na rangi ya sauce)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hakikisha unaongeza au kupunguza viungo kutokana na mahitaji yako.

misosi-chicken-tandoori0

 • Andaa kuku, kata vipande vinavyotosha kisha osha vizuri. Usitoe ngozi ili isaidie nyama kuiva vizuri wakati wa kuoka. Nyunyizia chumvi kwenye kuku. Hifadhi pembeni.
 • Andaa marinade. Kwenye bakuli – kamua limao au ndimu,  weka kitunguu saumu, tangawizi na tandoori sauce. Koroga vizuri hadi vichanganyike vizuri. Chovya vipande vya kuku kimoja baada ya kingine kwenye marinade. Hakikisha umepaka sauce vizuri kwenye nyama, kati ya nyama na ngozi. Rudia vipande vyote hadi umalize. Unaweza pia kuloweka vipande kwenye sauce kama iko nyingi. Hifadhi nyama kwenye jokofu kwa muda wa saa 1 hadi 2 ili viungo vipate kuingia vizuri.
 • Washa oven, weka nyuzijoto 200°C (392°F) kwa muda wa dakika 10.
 • Paka mafuta kiasi juu ya nyama na kati ya ngozi na nyama. Mafuta yanasaidia kuifanya nyama iive bila kukauka na kuwa ngumu.
 • Panga nyama vizuri kwenye wavu wa kuokea, hakikisha kuna nafasi vizuri kati ya nyama. Weka nyama kwenye oven, tega muda wa dakika 50 hadi 60 ili nyama ipate kuiva. Kama oven inatoa joto chache kwa chini, geuza nyama kila baada ya dakika 15 ili iive vizuri  pande zote.
 • Baada ya dakika 50 hadi 60 angalia kama nyama imeiva vizuri na imechuja maji yote. Epua na hifadhi pembeni.

Wakati kuku anaokwa, andaa sauce

 • Andaa kitunguu maji na kitunguu saumu – menya kisha kata vipande vidogo. Osha kisha kata pilipili hoho na cayenne pepper vipande vidogo. Menya kisha kata karoti kwenye vipande vidogo. Osha bamia, kata ncha kisha kata vipande vidogo unavyopenda, au unaweza pia kuacha ziwe nzima. Hifadhi pembeni.
 • Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto, kisha weka mafuta ya kula. Yakipata moto, weka kitunguu saumu, kitunguu maji. Koroga vizuri hadi viive. Weka bamia, koroga kisha acha iive kwa dakika 3. Weka nyanya fresh, koroga pamoja. Acha zichemke kwa dakika angalau tano, ili zilainike. Baada ya kuiva, weka nyanya ya kopo. Koroga pamoja, funika acha viive. Baada ya dakika 3 hadi 5, weka pilipili hoho, karoti na cayenne pepper kisha koroga pamoja. Acha viive. Koroga kisha funika kidogo viive vizuri -takribani dakika 3.
 • Kuku akishaiva, weka kwenye sauce iliyo jikoni. Koroga vizuri, unaweza kuongeza maji, tui la nazi au maziwa kidogo ili kuipa ladha. Funika vizuri, acha ichemke kwa dakika 5 hadi 7. Ikishaiva, epua na weka pembeni.
 • Unaweza kula mboga hii na chakula chochote upendacho – ugali, wali, ndizi, couscous au unachopendelea. Jirambe kwa raha zako.

misosi-kuku-main-0


MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa kuoka
saa 1
Walaji: 4

Salad yenye sausage
dakika 5
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.