Half cakes zenye maziwa, iliki, mayai na mdalasini

Half cake ni kitafunwa kilichozoeleka na watu wengi. Ni kitu pekee ambacho unaweza kukipata bila matatizo – dukani au gengeni. Je wewe unajua kuandaa ? Mara nyingi half cake unazonunua hazina utamu mzuri kama huu sababu hazina vitu vingi. Andaa pishi hili ili uweze kula kitu tofauti chenye ladha zaidi ili ufurahi na familia yako.

Mahitaji

 • Unga wa ngano kilo 1
 • Sukari vikombe viwili
 • Baking powder kijiko 1 na nusu kidogo
 • Mdalasini kijiko kidogo 1
 • Tangawizi ya unga kijiko 1 cha chai
 • Iliki nusu kijiko cha chai
 • Chumvi robo kijiko kidogo
 • Vanilla kijiko kidogo 1 
 • Mayai 2
 • Maziwa kikombe 1
 • Butter isiyo na chumvi vijiko 4 vikubwa
 • Mafuta
 • Baking soda nusu kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kama ni kwa chai, kula mchana au jioni, half cakes zinaenda tu. Ni kitu rahisi kuandaa, uwepo wa ngano huzifanya kushibisha vizuri na kwa muda mrefu. Vilevile, ni rahisi kuhifadhi na unaweza kula kwa muda mrefu, cha muhimu ujue tu jinsi ya kuhifadhi.

 • Weka unga, baking powder, baking soda, sukari, mdalasini, tangawizi, chumvi na iliki kwenye bakuli. Changanya vizuri. Weka siagi (butter) kisha changanya vizuri hadi butter ipotelee kwenye unga – unaweza kutumia vifaa au hata mikono inafaa tu, hakikisha umeosha na misafi.
 • Tengeneza kama shimo katikati ya unga, weka mayai na vanilla, changanya pamoja. Weka maziwa kiasi kwa awamu huku ukiendelea kukanda. Kanda vizuri hadi dida (Unga uliokandwa) liwe laini. Ukimaliza, funika na weka dida sehemu yenye joto ili uumuke. Acha kama dakika 40. Baada ya huo muda, Sukuma kwenye kibao kisha kata vipande vya wastani ukubwa wa keki unayopendelea  na uchome kama unavyopika maandazi.
 • Unaweza kula half cake na maharage, chai, supu au kama kitafunwa cha kawaida.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kachori
dakika 20
Walaji: 4

Grilled Tandoori Chicken Sauce
dakika 75
Walaji: 4

Tortilla Sandwich
dakika 25
Walaji: 2

Pilipili
dakika 15
Walaji: 5

Toa maoni yakoThomas
07:52, Sat 09 Jul 2016

Napenda sana kujipikia chakula changu mwenyewe

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.