Jinsi ya kuandaa unga wa kupikia vitafunwa tofauti

Hii ni njia rahisi ya kuandaa dida la kupika vitafunwa ambavyo haviitaji kuokwa kwa muda mrefu. Unaweza kutumia dida hili kupika chochote unachotaka.

Mahitaji

  • Unga wa ngano vikombe 2
  • Maji ¾ kikombe
  • Kijiko 1 cha chumvi
  • Siagi (butter) ¾ kikombe

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hii ni njia rahisi ya kuandaa dida la kupika vitafunwa ambavyo haviitaji kuokwa kwa muda mrefu. Unaweza kutumia dida hili kupika chochote unachotaka.

  • Changanya unga na chumvi katika bakuli kubwa (au katika bakuli ya mashine ya umeme ya kuchanganyia (food processor)). Weka maji kwenye unga kwa awamu huku unakoroga hadi maji na unga yawe sawia na unga uache kunata kwenye kuta za bakuli. Weka unga kwenye umbo la mpira, acha kwa dakika 10.
  • Weka siagi kwenye karatasi, funga vizuri kisha iponde hadi ilainike. Hifadhi kwenye jokofu hadi iwe ngumu, itachukua kama dakika 20.
  • Nyunyiza unga kiasi kwenye sehemu unatakayokandia. Weka unga uliochanganywa maji (dida), tengeneza umbo la mstatili, kisha weka siagi juu yake – iwe eneo la kati tu. Kunja dida kwenye sehemu tatu zilizo sawa huku ukifunika siagi na dida la unga. Ukimaliza, sukuma unga kwa kutumia mche wa kusukumia chapati. Ukishakaa kwenye umbo paba, kunja tena mara tamu kama mwanzo. Weka dida kwenye mfuko wa plastiki na hifadhi kwenye jokofu kwa dakika 30.

pastry-misosi1

pastry-misosi2

pastry-misosi3

pastry-misosi4

  • Rudia kusukuma unga, kunja mara mbili zaidi, halafu rudisha kwenye jokofu hadi unga uwe umetengemaa. Unga ukishatoka, rudia tena hizi hatua mara mbili ili iwe mara 6, halafu rudisha kwenye jokofu.
  • Unga utakuwa tayari kutengeneza kitu chochote unachopenda.

 


MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi za mayai
dakika 15
Walaji: 4

Biryani ya nyama
dakika 45
Walaji: 6

Ndizi utumbo za nazi
dakika 45
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.