Juisi ya chungwa na asali – kinywaji cha moto

Usipagawe kuona juisi ya moto, kama hujawahi kunywa basi jaribu hii. Huwezi kujutia. Ni kinywaji murua kwa wakati wa kupumzika jioni ukiwa unatafakari maisha. Ni kinywaji mbadala asubuhi kwa chai, maana hunywewa kikiwa cha moto na hakuna sukari inayoongezwa bali asali ambayo haina madhara mwilini. Kuwa makini maana asali huwa inakufanya upate usingizi kirahisi.

Mahitaji

  • Juice ya chungwa (Unaweza kukamua au ukatumia ya box)
  • Asali ya nyuki
  • Chombo cha kuchemshia ( sufuria, glass au bilauri)
  • Microwave au jiko la kawaida

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

  • Unaweza kuandaa juisi hii kwa kuchanganya asali na juisi na kisha kuipasha moto.
  • Kama unatumia microwave changanya juisi na asali na kisha weka kwenye microwave kwa muda wa dakika 1 hadi 2 ili ipate kuchanganyika vizuri.
  • Kama huna microwave, changanya asali na juisi kisha weka kwenye sufuria na bandika jikoni kwa muda wa dakika 5 hadi 7. Acha ichemke vizuri ili asali na juisi zichanganyike vizuri. Unaweza kukoroga pia ili kusaidia mchanganyiko uwe sawia.
  • Asali ikiwa kwenye microwave inapata kulainika, hivyo huchanganyika vizuri na juisi na kuipa utamu wa kipekee. Kwa maana hiyo unaweza pia kutumia asali yenye mabonge maana italainika vizuri, kwani microwave pia hutumika kulainisha asali.

Tahadhari: Kama unatumia microwave hakikisha hutumii sufuria au kitu chochote cha bati (kijiko, uma, kisu nk) maana ni hatari na unaweza kusababisha mlipuko. Ni vizuri kama utatumia bakuli za udongo au glass kutengeneza huu mchanganyiko.


MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi utumbo za nazi
dakika 45
Walaji: 4

Tembele
dakika 10
Walaji: 4

Mishikaki ya kupaka
dakika 45
Walaji: 3

Chicken fried rice
dakika 10
Walaji: 2

Toa maoni yakomama
00:58, Tue 29 Apr 2014
Kwakweli ngoja na mimi nijaribu mana nina machungwa mengi leo
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.