Juisi yenye karoti, chungwa na peach

Juisi ni chakula bora na kinachopendwa na watoto. Hakikisha mtoto wako hanywi juisi za viwandani, maana juisi bora zaidi ni ile inayotengenezwa kwa kutumia matunda moja kwa moja bila kuchanganywa na kemikali. Hii juisi ina mchanganyiko wa matunda 3 ambayo yanatoa virutubisho vingi na muhimu mwilini.

Mahitaji

 • Machungwa 3
 • Karoti 2
 • Peach 1
 • Asali (ONYO: USITUMIE ASALI KWA MTOTO CHINI YA MWAKA MMOJA)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kamua chungwa vizuri kisha hifadhi kwenye chombo safi pembeni.
 • Menya karoti kisha kata vipande vidogo vidogo. Weka kwenye jagi la kusagia  (blender).
 • Menya peach, kata vipande vidogo vidogo kisha toa mbegu. Changanya na karoti kwenye jagi.
 • Changanya juisi ya chungwa kwenye jagi, hii inasaidia kutumika kama kilainishi.
 • Saga vizuri hadi vipondeke na kuwa laini kabisa.
 • Tumia chujio, chuja juisi vizuri kwenye chombo safi, mfano bakuli.
 • Mie nimeongeza asali, lakini siyo lazima kuongeza asali, maana juisi kama ilivyo ni tamu. Kabla hujaongeza asali zingatia umri wa watoto wanaokunywa hii juisi.

ZINGATIA: Usimpe asali mtoto mwenye umri chini ya mwaka mmoja. Asali huweza kubeba vijidudu hatarishi kwa mtoto mchanga ambavyo husababisha ugonjwa unaoitwa Botulism.

UMUHIMU

Juisi hii ina mchanganyiko wa matunda, hivyo ina virutubisho vingi zaidi vya asili. Kati ya faida chache ni kama hizi:

 • Chanzo cha vitamin C (Chungwa)
 • Kuboresha kinga ya mwili (Peach)
 • Kuifanya ngozi kunawiri (Peach, karoti)
 • Kuimarisha moyo na macho (Peach, karoti)
 • Kusafisha damu (Chungwa, karoti)
 • Kuboresha mmeng’enyo wa chakula (Karoti)

MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi na mayai
dakika 10
Walaji: 1

Samaki wa ngano na tangawizi
dakika 15
Walaji: 2

Kuku wa limao
dakika 45
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.