Kababs za kuku na mayai

Kababs za kuku kwa maelezo rahisi na matokeo mazuri. Ni chanzo kizuri cha protini kutoka kwenye nyama ya kuku na mayai. Uwepo wa viungo unafanya kababs kuwa na harufu nzuri, zinavutia na kuleta vionjo vitamu wakati wa kula.

Mahitaji

 • Minofu ya kuku ½ kilo (changanya kidali na paja)
 • Kitunguu maji 1, kata vipande vidogo
 • Bizari nyembamba ya unga kijiko 1 cha chai
 • Giligilani ya unga ½ kijiko cha chai
 • Pilipili manga ya unga ¼ kijiko cha chai
 • Garam masala kijiko 1 cha chai
 • Limao kijiko 1 cha chai
 • Pilipili ndefu 3
 • Giligiliani za majani vijiko 4 cha chai
 • Tangawizi kijiko 1 cha chai
 • Kitunguu saumu kijiko 1 cha chai
 • Yai 1
 • Viungo vya kuku – chagua unavyopenda
 • Cheese iliyokwanguliwa vijiko 2 vya chakula
 • Mafuta ya kula
 • Mint fresh kijiko 1 cha chakula
 • Chumvi kijiko 1 cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kwa matokeo mazuri ya kababs changanya minofu itokayo kwenye kidali na paja la kuku. Hizi nyama zina kiwango kidogo cha mafuta ambayo yatatoa nyama iliyonona zaidi.

 • Kama unatumia vijiti vya mbao kuandaa hizi kababs ni vizuri kuziloweka kwenye maji kwa muda wa masaa 2 hadi 3 ili kuzuia zisiungue wakati wa kuchoma kababs.

wooden-skewers11

 • Safisha nyama ya kuku kisha kausha maji. Kama nyama haina mafuta unaweza kuongeza kijiko 1 cha siagi (butter) kwenye nyama.

kebab-ingredient

kebab-ingredients

 • Menya kitunguu na kisha saga kwenye mashine ya kusagia chakula (blender), saga kiasi lakini kisilainike sana. Toa kitunguu, chuja maji yote kisha rudishia kwenye blender. Weka pilipili, majani ya giligiliani, mnanaa (mint), chumvi, tangawizi, kitunguu saumu, bizari nyembamba, pilipili manga, garam masala, limao, giligilani ya unga na viungo vya kuku. Saga mchanganyiko ili uchanganyikane vizuri ila usisage kupita kiasi ili ubaki na minofu ya kuku kwa mbali.
 • Weka mchanganyiko kwenye bakuli safi. Pasua yai, koroga pembeni. Mimina kidogo kidogo kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa nyama  huku ukiwa unakoroga. Mchanganyiko ukianza kuwa mwepesi acha kuweka yai.
 • Kwangua cheese na weka kwenye mchanganyiko ili kuongeza ladha. Funika bakuli, weka kwenye jokofu kwa muda usiopungua masaa 2 ili viungo vipate kufanya kazi yake na mchanganyiko ushikane ili iwe rahisi kutengeneza umbo unalotaka.
 • Ukiwa unahitaji kupika, tengeneza maumbo unayopendelea – mipira, au kama umbo la sausage kwenye mti wa mshikaki. Hakikisha una maji pembeni, osha mikono, chovya kwenye maji kiasi na kisha tengeneza umbo unalohitaji.

kebab-shaped

 • Unaweza kupika hizi kababs kwenye oven au kwenye kikaango cha kawaida. Kama unatumia oven, washa oven kwenye nyuzijoto 200°C na acha ipate moto vizuri. Panga kababs kwenye waya wa kuchomea, kisha weka kwenye oven kwa muda wa dakika 10. Kama oven haitoi joto sawia, geuza mara kwa mara ili kababs ziive vizuri.
 • Kama unatumia kikaango. Paka mafuta (mfano: siagi) kwenye kikaango, ikipata moto vizuri panga kabab na pika kwa dakika 10 au zaidi. Pika huku ukigeuza kila upande kuhakikisha zinaiva na kupata  rangi ya kahawia.

kebab-smokey-with-charcoal

 • Epua, hakikisha kababs zimeiva vizuri na ujirambe.

misosi-kababs-main


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.