Kabeji yenye royco

Kabeji ni chanzo kizuri cha vitamin A, C, ufumwele, madini ya Calcium na magnesium. Ni mboga rahisi kuandaa na tamu wakati wa kula. Andaa mboga hii ili ufurahie wewe pamoja na familia

Mahitaji

  • Kabeji nusu
  • Kitunguu maji 1 kikubwa
  • Royco kijiko 1 cha chai
  • Mafuta ya kula vijiko 2
  • Karoti 1
  • Chumvi kijiko 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

  • Andaa kabeji kwa kukata kwenye saizi unayopenda. Osha vizuri, chuja maji. Menya karoti, kisha changanya na kabeji.
  • Bandika sufuria jikoni, ikipata moto weka mafuta. Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji huku unakoroga taratibu. Kitunguu kikiiva weka kabeji na chumvi. Pika kwa moto mkali kwa dakika 5. Weka royco na koroga kwa dakika 3 hadi 5 kisha epua.
  •  Jirambe na mboga tamu ya kabeji. Unaweza kula hii mboga na ugali au vyakula vingine uvipendavyo.

kabeji-misosi-poor


MAPISHI YAPENDWAYO

Kababs za kuku na mayai
dakika 20
Walaji: 4

Macaroni ya bilinganya na nazi
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.