Kachori

Mahitaji

 • Viazi ulaya 10
 • Chumvi kiasi
 • Pilipili ya unga vijiko 2 vya chai
 • Unga wa ngano kikombe 1
 • Vitunguu maji 3
 • Saumu ya unga kijiko 1 cha chai
 • Giligilani kiasi
 • Mafuta
 • Ndimu unavyopenda

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya viazi,weka chumvi kisha bandika jikoni. Vikiiva epua, weka ndimu na pilipili ya unga viponde ponde kisha weka pembeni.
 • Chukua kitunguu, menya kikwangue kwenye kifaa cha kukwangulia karoti, weka kwenye viazi ulivyo ponda ponda weka saumu na giligilani kisha changanya.
 • Changanya vizuri, chukua mchanganyiko wa viazi kisha tengeneza maduara yenye ukubwa kiasi, weka pembeni. Rudia mpaka mchanganyiko wote uishe.
 • Chukua unga wa ngano, changanya na maji ili upate uji ambao sio mzito sana wala mwepesi sana, chukua yale madongo yachonywe kwenye huo uji kisha choma kwenye mafuta.
 • Rudia mpaka kachori zote ziishe, hakikisha zinaiva na kua rangi ya kahawia. Epua kisha jirambe. Unaweza kula na chai, soda au chochote utakachopenda.

MAPISHI YAPENDWAYO

Wali wenye nazi na maziwa
dakika 20
Walaji: 2

Nyama tamu yenye pilipili
dakika 25
Walaji: 4

Mishikaki mitamu yenye papai
dakika 30
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.