Kachori tamu zenye giligilani

Kachori ni kitafunwa kizuri na rahisi kuandaa nyumbani. Kachori hizi ni tamu kutokana na uwepo wa viungo vinavyokupa harufu tamu na ladha bora. Chukua muda mchache, andaa kachori hizi ili kuwapa raha wale uwapendao.

Mahitaji

 • Viazi mbatata 10
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Pilipili ya unga vijiko 2 vya chai
 • Unga wa ngano kikombe 1
 • Vitunguu maji 3
 • Kitunguu saumu cha unga kijiko 1 cha chai
 • Giligilani  kijiko 1 cha chai
 • Mafuta ya kula (Nimetumia olive oil)
 • Ndimu unavyopenda

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza mahitaji kutokana na unavyopenda.

 • Andaa viazi - menya kisha weka kwenye sufuria, ongeza maji na chumvi kisha bandika jikoni. Acha vichemke havi viive. Epua. Hakikisha unakata viazi na kuviweka kwenye maji ili visipate ukungu wa rangi nyeusi juu yake.
 •  Weka ndimu na pilipili ya unga kwenye viazi. Ponde hadi vilainike na kuwa uji mzito. Weka pembeni.
 • Menya na kwangua kitunguu kwa kutumia kifaa cha kukwangulia karoti. Weka kitunguu kwenye viazi ulivyoponda. Weka pia kitunguu saumu na giligilani. Changanya pamoja.
 • Finyanga umbo la mipira yenye ukubwa wa wastani kwa kutumia mchanganyiko wa viazi. Hifadhi kwenye  chombo safi pembeni. Rudia hatua hii hadi umalize mchanganyiko wote.
 • Bandika sufuria au kikaango jikoni, weka mafuta na weka moto uwe mkali ili mafuta yapate moto vizuri.
 • Changanya unga wa ngano na maji ili upate uji wenye uzito wa wastani. Chovya viazi ulivyofinyanga kwenye mchanganyiko wa ngano. Hakikisha mchanganyiko wa ngano umejaa vizuri kwenye mpira va viazi. Kaanga kwenye mafuta yaliyopata moto vizuri. Weka kachori zinazotosha lakini usirundike sana ili kuzipa nafasi ya kuiva vizuri na kwa nafasi.
 • Rudia hatua hii hadi kachori zote ziishe. Hakikisha kachori zinaiva na kuwa rangi ya kahawia kabla ya kuzitoa.
 • Epua, hifadhi pembeni. Unaweza kula kachori hizi na chai, kinywaji baridi, au kama kitafunwa cha kawaida. Jirambe na kachori tamu.

misosi-kachori-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Mishikaki mitamu yenye papai
dakika 30
Walaji: 6

Kababs za kuku na mayai
dakika 20
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.