Kamba wenye mboga za majani

Mchanganyiko wa kamba (prawns) na mboga za majani ni kitoweo kizuri cha haraka. Mboga hii inaweza kuwa tayari kwa muda mchache lakini unapata ladha tamu yenye virutubisho vingi sana. Karibu tujirambe huku tukiwa tunajenga afya.

Mahitaji

 • Kamba (prawns) gramu 100 (Tumia kiwango unachohitaji)
 • Pilipili hoho 2 (nimetumia zenye rangi tofauti ili kuleta rangi nzuri)
 • Chumvi
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu
 • Pilipili manga

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mboga rahisi kuandaa kwa matokeo mazuri. Ni mboga mahsusi kwa kuandaa kama ukiwa huna muda mwingi wa kukaa jikoni lakini unapenda matokeo mazuri yenye kuwapa wale uwapendao tabasamu la bashasha wakati wanaendelea kujiramba mezani. 

misosi-prawns-mbogamboga

 • Andaa kitunguu maji – menya kisha kata vipande vidogo. Menya kisha saga kitunguu saumu. Kata pilipili hoho kwenye vipande vidogo. Hifadhi pembeni.
 • Andaa kamba (prawns) kwa kutoa magamba. Osha kisha nyunyizia limao na chumvi. Weka kitunguu saumu. Acha kamba wakae kwa dakika 5 hadi 10 ili kitunguu saumu kiingie vizuri.
 • Bandika kikaango jikoni, weka mafuta kidogo sana. Yakipata moto, weka kamba. Ivisha upande mmoja kwa dakika 2 hadi 3 kisha geuza upande wa pili. Epua na weka pembeni.
 • Punguza moto kiasi. Bandika kikaangio jikoni, weka mafuta kiasi. Yakipata moto weka kitunguu maji. Koroga kiasi. Acha kiive hadi kianze kubadilika rangi. Weka pilipili hoho, koroga vizuri. Weka kamba, kisha koroga vizuri taratibu. Unaweza kuongeza kionjo tofauti ili kuleta ladha – mie nimeongeza mchuzi mix kidogo sana ili kuleta ladha na harufu nzuri.
 • Unaweza kula hii mboga na vyakula tofauti – ugali, tambi, wali nk
 • Jirambe.

misosi-prawns-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Nyama ya kuoka na ndizi mzuzu
dakika 45
Walaji: 2

Kuku wa kuoka na tambi
dakika 45
Walaji: 2

Mboga ya majani mchanganyiko
dakika 10
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.