Karanga za mayai

Karanga za mayai ni nzuri mana zinatupatia virutubisho vingi muhimu. Unaweza kula kwa kimiminika chochote au ukala zenyewe na ukazifurahia.

Mahitaji

 • Karanga kilo 1
 • Yai moja
 • Mafuta ya kula ( ya maji ) mls 750
 • Sukari vijiko 6 vya chakula
 • Unga wa ngano kikombe kimoja cha kahawa( coffee cup)
 • Chumvi ya unga nusu kijiko cha chai.
 • Jiko
 • Chombo –Sufuria/bakuli
 • Mwiko /kijiko kikubwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chukua  yai,  pasua  na  koroga  kwenye  chombo  kisafi. 
 • Chukua  karanga,mimina kwenye chombo ulicho koroga yai ,changanya kwa kutumia mikono.
 • Weka chumvikidogo, changanya vizuri, weka sukari changanya, mimina unga wa ngano, changanyavizuri.
 • Weka mafuta jikoni hadi yapate moto.
 • Chota karanga kwa kutumia kijiko  kikubwa  na  weka  kwenye  mafuta  kisha  zigeuze  bila  kuacha  hadi utakapoona karanga zimebadilika rangi kua kahawia.
 • Tumia  kijiko  kikubwa  kuziepua  na  weka  kwenye  chombo  kisafi  cha  wazi  ilizipoe.
 • Funga kwenye vifuko vidogo na zihifadhi mahali pasafi tayari kwa kula au kuuza.

MAPISHI YAPENDWAYO

Viazi na meatballs za nazi
dakika 20
Walaji: 4

Tambi za mayai
dakika 15
Walaji: 4

Biryani ya nyama
dakika 45
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.