Cutlets za pilipili

Cutlets inatakiwa kupikwa na nyama laini inayoiva haraka. Hizi cutlets unaweza kuzila kwa wali au chakula kingine; unaweza pika kutafuna kwa hamu mdomoni kama wajisikia haja ya kula kitu kitamu.

Mahitaji

 • Nyama ya kusaga Kilo 1
 • Viazi mbatata 8
 • Giligilani
 • Kitunguu saumu kijiko 1 cha chai
 • Tangawizi kipande kidogo
 • Pilipili hoho 1
 • Karoti 1
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Ndimu kiasi
 • Bizari nyembamba ya kusaga kijiko 1 kidogo
 • Pilipili manga nusu kijiko kidogo
 • Mayai 2
 • Unga wa ngano robo kikombe
 • Mafuta ya kula
 • Ndimu kiasi
 • Kitunguu maji 2
 • Pilipili ndefu 2

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kwenye sufuria weka nyama ya kusaga, chumvi kiasi, ndimu, kitunguu saumu, na tangawizi kisha bandika jikoni. Usiweke maji kabisa, acha iive yenyewe na maji yake. Pika nyama huku ukikoroga mara kwa mara. Ikishakuwa tayari, epua weka pembeni ipoe. Ni vizuri ukionja ili ujue kama viungo viko sawa.
 • Menya Viazi, weka kwenye sufuria, ongeza maji na chumvi kisha bandika jikoni. Viazi vikiiva chuja maji na viponde ili vilainikie halafu hifadhi pembeni.
 • Osha kisha kata pilipili hoho, vitunguu maji, karoti, na pilipili ndefu kwenye vipande vidogo, hifadhi pembeni.
 • Weka mchanganyiko wa nyama na viazi katika chombo kimoja kisha weka vitunguu maji, pilipili hoho, karoti na pilipili juu yake. Weka pia kitunguu saumu, kamulia ndimu, unga wa bizari nyembamba,  pilipili manga, katia na giligilani. Changanya vyote kwa pamoja hadi mchanganyiko uwe sawia. Unaweza kuonja ili kujua kama chumvi inatosha.
 • Kwa kutumia mchanganyiko huu, tengeneza mabonge yenye maumbo ya ukubwa unaopenda, inaweza kuwa umbo la yai au duara, kisha hifadhi pembeni. Rudia hatua hii hadi mchangayiko wako wote uishe.
 • Changanya unga wa ngano na maji. Mchanganyiko uwe mzito kisha weka mayai. Changanya vizuri unga na mayai hadi, hifadhi pembeni.
 • Weka kikaango (frying pan) jikoni. Weka mafuta ya kula ya kutosha, acha yapate moto vizuri sana.
 • Chovya mabonge ulivyoandaa katika unga uliochanganywa na mayai kisha tumbukiza kwenye mafuta yaliyopata moto vizuri. Usirundike vipande vingi kwenye mafuta, maana havitoiva vizuri. Pika kwa awamu na utarabitu mzuri. Acha hadi vipande vibadilike rangi kisha epua. Rudia hadi vipande vyote viishe. 
 • Unaweza kula cutlets hizi na vitu tofauti - kama mboga, vitafunwa na namna unayopenda. Jirambe na utamu wa cutlets za pilipili.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kabeji yenye royco
dakika 10
Walaji: 4

Samaki wenye sauce ya pilipili
dakika 35
Walaji: 4

Maandazi ya apple
dakika 5
Walaji: 5

Tambi za maziwa na iliki
dakika 15
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.