Kebab za nyama

Unaweza kuandaa kebab hizi kwa kutumia nyama ya samaki, kuku au ya ngombe. Kebab hizi zinaweza kuliwa kama kiambato cha chakula kikuu, lakini pia unaweza kula kama kitoweo kwa vinywaji tofauti – ni ubunifu wako tu.

Mahitaji

 • Fillet za nyama ya ng’ombe, kuku au samaki (Tuna)
 • Yai 1
 • Slice ya mkate 1
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Karafuu iliyosagwa
 • Chumvi
 • Limao
 • Coriander

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa vitunguu – pilipili hoho, kitunguu saumu na kitunguu maji – menya na kata vipande vidogo. Ponda kitunguu saumu kwenye kinu.
 • Andaa nyama (samaki, kuku au ya ng’ombe) kwa kuikata vipande, kuiosha na kisha kuichemsha.
 • Weka ndimu na chumvi kwenye nyama.
 • Nyunyuzia pilipili manga
 • Usiongeze maji kwenye nyama. Acha ikauke.
 • Nyama ikikauka, weka kitunguu.
 • Loweka slice ya mkate kwenye maji. Itoe na ikamue kisha changanya na mayai lililopasuliwa na kukorogwa na coriander. Hakikisha mchanganyiko umejichanganya vizuri.
 • Injika kikaangio jikoni. Weka mafuta mengi kiasi. Subiria yachemke.
 • Tengeneza umbo la uviringo kutoka kwenye nyama,samaki au kuku kisha chovya kwenye rojo la mkate na mayai .
 • Tumbukiza mchanganyiko kwenye mafuta. Ingiza kimoja baada ya kingine. Ili kupata matokeo mazuri, ingiza kwenye mafuta, huku ukitumia mshikio, weka mchanganyiko ndani ya mafuta kwa muda wa sekunde 5 – 8 ili kujenga koti na kuwezesha kuiva vizuri.
 • Rudia hatua hii kwa vipande vyote vilivyobaki.
 • Ipua vile vilivyoiva na subiria vikauke – unaweza kujiramba

MAPISHI YAPENDWAYO

Grilled salmon
dakika 40
Walaji: 2

chilli chicken
dakika 30
Walaji: 3

Nyama ya kuoka na ndizi mzuzu
dakika 45
Walaji: 2

Toa maoni yakojane
08:39, Sun 01 Feb 2015

asante kwa kutufundisha mapishi.kaz nzuri inatusaidia .MUNGU AKUPE MWISHA MAREFU.BIG UP

Dadia Msindai
13:31, Mon 02 Feb 2015

@Jane, asante sana kwa baraka zako, Mungu akubariki pia kwa upendo wako. Nafurahi kama umefurahia mapishi. Karibu tuendeleze afya njema kwa kila mmoja wetu.

Sifa yuauf
14:16, Tue 16 Jun 2015

Napenda sana maelekezo yako sababu hayaitaj gharama..mfano kwenye mkate niliambiwa ninunue chenga special wakat kumbe unaeza tumia hata slice..endelea na moyo huo.

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.