Keki tamu ya mtindi na vanilla

Hii keki ni rahisi sana kuandaa maana hahihitaji ujuzi mwingi na inachukua muda mfupi na ina faida nyingi zaidi kwa afya yako kutokana na uwepo wa mtindi na mdalasini. Unapata ladha tamu, mwili wako unapata virutubisho na pia unafurahia harufu nzuri ya vanilla inayokuvutia zaidi kwenye keki.

Mahitaji

 • Siagi (butter) ½ kikombe
 • Vikombe 2 vya unga wa ngano
 • Sukari kikombe 1
 • Kijiko 1 cha baking soda
 • Baking powder ½ kijiko
 • Kijiko 1 cha mdalasini
 • Kijiko 1 cha vanilla
 • Kijiko 1 cha
 • Mayai 2
 • Kikombe 1 cha mtindi (Yogurt)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongeza au kupunguza mahitaji kulingana na unavyopendelea.  Unaweza pia kuweka chocolate ya unga kiasi ili kuipa keki ladha zaidi.

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 175°C (350°C).  Acha ipate moto wakati unaandaa mchanganyiko wa keki.
 • Kwenye bakuli kubwa – changanya pamoja siagi, sukari na vanilla. Koroga vizuri hadi mchanganyiko uwe sawia. Pasua yai, weka kwenye mchanganyiko. Koroga pamoja hadi mchanganyiko uwe laini.
 • Changanya unga, baking soda na baking powder. Koroga pamoja.
 • Kwa awamu, weka mchanganyiko wa unga kiasi kwenye mchanganyiko wa siagi na mayai kisha koroga vizuri kwa pamoja.  Kisha weka mtindi kiasi kwenye mchanganyiko wa siagi na mayai, koroga vizuri. Fanya hivyo hadi unga na mtindi wote uwe umechanganyikana vizuri na kuacha mchanganyiko ulio sawia.
 • Andaa chombo cha kuokea keki kwenye oven (au sufuria kama unapika kwenye jiko la mkaa) kwa kukipaka mafuta na unga vizuri. Miminia mchanganyiko wa keki kwenye chombo cha kuokea.
 • Weka kwenye oven. Tega muda wa dakika 50. Baada ya dakika 50 chomeka kijiti au kisu kwenye keki ili kuangalia kama imeiva. Kikitoka kikavu, keki imeiva, weka pembeni ipoe kiasi kabla ya kula.
 • Unaweza kula keki hii kama upendavyo – kama kisindikiza mlo, kwa kinywaji baridi au vinginevyo. Jirambe kwa ladha tamu ya keki hii ya mtindi.

misosi-yoghurt-cake

mtindi-cake-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Kashata za nazi
dakika 12
Walaji: 5

Kashata za nazi
dakika 12
Walaji: 5

Pizza yenye sausage topping
dakika 15
Walaji: 1

Togwa
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.