Keki ya chocolate

Kuandaa vitu vitamu, hasa kuoka mikate, cake, maandazi na vingine ni wakati murua sana kupitisha muda wangu. Niliwahi kuonja hii keki kabla ya kuuandaa, na sikuweza kujizuia, ikabidi niandae tu ili nipate kuhisi tena ile ladha tamu. Hakika familia ilifurahia na tulijiramba hasa. Ni keki iliyo bora, rahisi kuandaa na hauhitaji ujuzi mkubwa sana, bali ni mapenzi yako na muda mchache sana. Jirambe na keki ya chocolate

Mahitaji

 • Unga vikombe 2
 • Sukari vikombe 2
 • Cocoa robo tatu ya kikombe
 • Baking powder vijiko 2 vya chai
 • Baking soda kijiko 1 na nusu cha chai
 • Espresso powder kijiko 1 cha chai
 • Maziwa kikombe 1
 • Mafuta nusu kikombe
 • Mayai 2
 • Chumvi kijiko 1 chai
 • Maji ya moto kikombe 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Pasha oven joto, weka nyuzi joto 350, vyombo unavyotumia kuoka keki vipake mafuta kisha weka pembeni.
 • Kwenye bakuli kubwa weka unga, sukari, cocoa, baking powder, baking soda, chumvi na espresso powder. Changanya vizuri mpaka mchanganyiko uchanganyikane vizuri.
 • Ongeza maziwa, mafuta na mayai kwenye mchanganyiko wa unga. Changanya mpaka uchanganyikane vizuri. Ongeza maji ya moto kisha changanya kwa dakika 2.
 • Weka mchanganyiko kwenye chombo cha kuokea, oka kwa dakika 30 mpaka 35. Epua chukua toothpick choma katikati kujua kama keki imeiva vizuri. Ikiwa tayari iache kwa dakika 10 ipoe. Itoe kwenye chombo cha kuokea kisha jirambe.

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.