Keki ya chocolate, maziwa na ndizi

Utamu wa hii cake ni zaidi ya maelezo. Uwepo wa chocolate unaifanya ivutie kwa macho, vanilla inaipa harufu tamu na utamu wake ni zaidi ya muonekano. Ni kitafunwa vizuri wakati wowote ili kuipa familia ladha tamu na mabadiliko.

Mahitaji

 • Unga wa ngano vikombe 2
 • Sukari kikombe 1
 • Ndizi 2, zilizoiva vizuri
 • Mayai 2
 • Mafuta ya kula ½ kikombe (Au butter 2/3 kikombe)
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Kikombe 1½ cha maziwa
 • Baking soda kijiko 1 kidogo
 • ½ kikombe cha cocoa ya kuokea (Au chocolate ya unga)
 • Vanilla flavor kijiko 1 kikubwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hii ni keki unayoandaa ukiwa na muda na hamu ya kula kitu kitamu, chenye afya na kinachoweza kukupa furaha. Ni muhimu kuandaa keki kama una muda mwingi wakati wa weekend, ili upate matokeo mazuri zaidi na kujumuika vizuri na familia.

 • Washa oven weka kwenye nyuzi 350°F (180°C). Acha ipate moto.
 • Kwenye bakuli kubwa, changanya butter na sukari hadi zichanganyike na kuwa laini. Ongeza mayai, moja baada ya jingine – pasua kisha changanya vizuri.
 • Kwenye chombo tofauti, changanya unga wa ngano, cocoa, vanilla flavor, baking soda na chumvi. Koroga vizuri. Changanya mchanganyiko huu kwenye bakuli lenye mchanganyiko wa mafuta na sukari. Kwenye chombo tofauti, ponda ndizi hadi zilainike vizuri kisha weka kwenye mchanganyiko wa unga na mafuta. Koroga vizuri.
 • Ongeza maziwa kidogo kwa wamu kwenye mchanganyiko huku unaendelea kukoroga vizuri. Rudia hadi maziwa yote yachanganyike vizuri.
 • Paka chombo unachotumia kuokea mafuta na unga vizuri, kisha mimina mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea.  Weka kwenye oven. Tega oven dakika 45 hadi 50. Jaribu kama cake imeiva – ingiza kijiti au kitu chembamba, kisha toa. Kikitoka kikavu, keki imeiva, kikitoka kimelowa, acha cake kwenye oven kwa muda wa dakika 10 zaidi. Kisha jaribu.
 • Ukishatoa cake kwenye oven, unaweza kuipaka chocolate juu yake ili ivutie zaidi. Mie sikupaka chocolate, maana uwepo wa chocolate ulikuwa unatosha.
 • Hii cake unaweza kula kama kitafwa kawaida, muda wowote unapohitaji kutafuna kitu.

misosi-cake-chocolate


MAPISHI YAPENDWAYO

Chocolate cake
dakika 40
Walaji: 6

Sambusa za nyama
dakika 15
Walaji: 10

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.