Keki ya mayai, vanilla na maziwa

Hii ni keki rahisi sana kuandaa lakini ni tamu kupita maelezo. Mapishi haya ya keki ni rahisi sana kupika na hayahitaji ufundi mkubwa sana. Unachotakiwa kufanya ni kuandaa vitu vizuri na kuacha mambo mengine yaendelee. Unaweza kuandaa keki hii kwa oven au kwa rice cooker. Jaribu kuandaa na uonje utamu wake.

Mahitaji

 • Kikombe 1½ cha unga wa ngano (kama gramu 200)
 • ½ kikombe cha siagi (margarine, kama gramu 133)
 • Mayai 2
 • Vijiko 2 vikubwa vya vanilla
 • Kikombe 1 cha sukari nyeupe (Ni kama gramu 200. Mie nimetumia mchanganyiko wa sukari nyeupe na brown)
 • Vijiko 1¾ vya hamira
 • ½ kikombe cha maziwa (maziwa ya maji)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hii ni keki rahisi sana kuandaa lakini ni tamu kupita maelezo. Mapishi haya ya keki ni rahisi sana kupika na hayahitaji ufundi mkubwa sana. Unachotakiwa kufanya ni kuandaa vitu vizuri na kuacha mambo mengine yaendelee. Unaweza kuandaa keki hii kwa oven, jiko la mkaa au kwa rice cooker. Jaribu kuandaa na uonje utamu wake.

20150124_214130

20150125_191551

 • Washa oven na weka kwenye nyuzi 350°F (180°C)
 • Paka chombo utakachotumia kuoka keki siagi (au mafuta) kwenye pande zote. (Mie huwa natumia foil paper, lakini ni vizuri utumie mafuta ili upate umbo zuri la keki yako)
 • Kwenye bakuli ya wastani, weka siagi na weka sukari. Changanya pamoja. Hakikisha vimekuwa laini na vimechanganyika vizuri. (Unaweza kutumia mashine ya umeme ya kuchanganyia, lakini hata kwa mkono inawezekana. Mie nimetumia whisk ya mkono tu kuchanganyia)

20150124_194016

20150124_194718

 • Gonga mayai, changanya kwenye mchanganyiko wako. Koroga hadi yachanganyike vizuri. Weka vanilla, koroga zaidi.

20150124_194747

20150124_195135

 • Kwenye bakuli tofauti, changanya unga na hamira. Koroga vizuri ili zipate kuchanganyika kwa ufasaha.

20150124_195711

 • Changanya mchanganyiko wa unga na hamira kwenye mchanganyiko wa mayai pamoja na sukari. Koroga vizuri ili vipate kuchanganyika sawia.

20150124_195925

 • Weka maziwa kwenye mchanganyiko na koroga vizuri hadi iwe laini na ichanganyike vizuri.

20150124_200019

20150124_200101

20150124_200241

 • Mwaga mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea. Kisha weka kwenye oven. Tega muda wa dakika 40 na usubirie.

20150124_200746

 • Baada ya dakika 40, toa keki, weka pembeni ipoe na kisha kata vipande ujirambe.

20150124_211111

20150124_214136

20150125_132845

20150125_191447


MAPISHI YAPENDWAYO

kisamvu cha nazi
dakika 30
Walaji: 4

Mapishi ya nyama ya kusaga
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoshufaa saidi
15:00, Mon 08 Feb 2016

uko powa.unafundisha vizuri sana

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.