Keki ya ndizi, chocolate na karanga

Nilijaribu kuandaa keki ya ndizi na karanga ili kuona ladha yake itakuwaje. Matokeo yake ni mazuri na nimefurahia keki. Kwenye hii keki kuna ndizi, vanilla, ngano, chocolate, siagi na sukari. Ni keki nzuri unayoweza kuipika na kuhifadhi kwenye jokofu na kuila wakati unapenda.

Mahitaji

 • Siagi (butter) 125g
 • Sukari 150g
 • Vanilla kijiko 1
 • Yai 1 egg, pasua na koroga vizuri
 • Ndizi 2 zilizoiva vizuri, zipondwe
 • Unga wa ngano vikombe 1½  
 • Maziwa ¼ kikombe (60ml)
 • Chocolate vijiko 3
 • Karanga zilizokaangwa 1/4 kikombe

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa keki ya ndizi, mayai, na chocolate. Tukimaliza mapishi yetu yataonekana kama hivi:

misosi-keki-ndizi

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 350°F (180°C)
 • Changanya siagi, vanilla na sukari kwenye kikaango au sufuria. Weka jikoni kwenye moto wa wastani. Acha siagi iyeyuke vizuri kisha epua.
 • Saga ndizi vizuri hadi ziwe uji, weka kwenye mchanganyiko wa siagi
 • Pasua mayai, changanya kwenye siagi na ndizi. Koroga vizuri. Weka chocolate na koroga pamoja vizuri.
 • Weka unga na maziwa kidogo kidogo kwa awamu kwenye mchanganyiko wa siagi huku unakoroga. Fanya hivi hadi umalize unga na maziwa.
 • Kwenye bakuli la kuoka – paka mafuta ya kula na unga kiasi ili mkate usinate kwenye chombo cha kuokea.
 • Mimina mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea na mwagia karanga kiasi juu yake ili ziwe zinaelea kwenye mchanganyiko wa unga. Kisha weka kwenye oven kwa dakika 35.
 • Baada ya dakika 35 toa mkate na weka kwenye sahani. Acha upoe na ukate kwa ajili ya kula.
 • Jirambe na ladha ya maisha.

keki-ndizi-misosi-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Supu ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yako



JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.