kisamvu cha nazi

Kisamvu ni mboga moja nnayoipenda kupita kiasi. Ni mboga ambayo hunipa ladha ya kipekee nikiipika na nazi halafu nakula pamoja na ugali. Huwezi kupinga kuwa mapishi haya yana upekee kwenye kukupa ladha halisi ya chakula cha kiafrika

Mahitaji

 •  Kisamvu
 • Kitunguu maji
 • Chumvi
 • Vitunguu swaumu
 • Nazi 2 (au unaweza kutumia karanga pia).

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 •  Chambua kisamvu na utwange kwenye kinu ukichanganya na vitunguu saumu mpaka kiwe laini
 • Kuna nazi na uchuje tui zito na jepesi
 • Kata vitunguu maji vipande vidogo
 • Anza kupika kisamvu chako hadi kiwe laini.
 • Kisamvu kikishaiva na maji kukauka, weka kitunguu maji na chumvi, kisha weka tui jepesi ilikiiendelee kuiva zaidi na kuwa laini
 • Tui likikauka weka tui zito na pika hadi tui likauke kabisa.
 • Unaweza kujiramba na mapishi yako

MAPISHI YAPENDWAYO

Vitumbua vya iliki na nazi
dakika 35
Walaji: 8

Dagaa wenye curry sauce
dakika 25
Walaji: 2

Sweet & Sour Chicken
dakika 45
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.