Koliflawa na nyama ya kusaga

Mboga hii ni nzuri kwa kula na wali mweupe. Ina mchanganyiko wa vazi, nyama ya kusaga, karoti, na viungo vingi kuipa ladha. Jaribu kuandaa ili kupata ladha maridhawa.

Mahitaji

 • Kitunguu maji 1
 • Vitunguu saumu 2
 • 1/4 kikombe cha mafuta ya kula
 • Kilo 1½ ya nyama   ya kusaga
 • Vijiko 2 chumvi
 • 1/2 kijikp cha pilipili manga iliyosagwa vizuri
 • Kijiko 1 cha unga wa curry
 • 1/2 kijiko cha coriander iliyosagwa
 • 1/2 kijiko cha bizari
 • 1/4 kijiko cha mdalasini
 • Karoti 1 iliyokata nyembamba
 • Viazi mviringo 2 vikakwa vipande vidogo
 • Koliflawa 1/2 ikatwe vipande vidogo
 • Vikombe 2 vya vitunguu vilivyopondwa
 • 1/2 kikombe cha maji

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kwenye kikaangio weka mafuta ya kula na acha yapate moto wastani. Ongeza kitunguu maji na koroga kiive. Wakati unakoroga, ongeza vitunguu saumu hadi vyote vianze kugeuka rangi ya udongo iliyopauka. Angalia visiungue.
 • Weka nyama ya kusaga pamoja na viungo vingine vilivyobaki. Koroga na pika nyama hadi iwe na rangi ya udongo.
 • Weka karoti, viazi, koliflawa, nyanya na maji. Weka moto wa wastani kisha funika acha vichemke.  Acha viive kwa muda wa dakika 25 hadi viazi view laini.
 • Onja na ongeza chumvi kama haitoshi. Unaweza kuweka pilipili kama unapenda.
 • Andaa wali wako na kula na sauce yako ya koliflawa na nyama ya kusaga.

MAPISHI YAPENDWAYO

Carrot cake
dakika 60
Walaji: 4

Grilled salmon
dakika 40
Walaji: 2

chilli chicken
dakika 30
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.