Koni za asali

Koni za asali ni vitafunwa vizuri, hasa kwenye nchi za kiarabu. Hii ni mojawapo ya vitafunwa vinavyopendwa sana Afrika kaskazini, hasa Algeria. Ni kitafunwa kinachoandaliwa kwa kutumia ngano, jamii ya karanga, maziwa na asali. Ni vitafunwa vizuri sana kwa kahawa au kwa chai. Ni rahisi kuandaa na pia unaweza kuhifadhi na kula unapohitaji.

Mahitaji

 • Vikombe 3 vya unga wa ngano
 • Siagi vijiko 2
 • Yai 1
 • Chumvi  ½ kijiko
 • Kijiko 1 cha vanilla
 • Mdalasini vijiko 2
 • Maji ya uvuguvugu, kulingana na mahitaji
 • Karanga (au korosho) 200 g
 • Hazelnut 200g
 • Maziwa 100mls
 • Matunda yaliyokaushwa, au unaweza kutumia machicha ya nazi.

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Ukimaliza kuandaa kitafunwa kitakuwa na muonekano kama huu

misosi-koni-asali

 • Changanya unga, chumvi, vanilla, siagi na yai kwenye chombo kinachotosha. Weka maji na changanya pamoja hadi mchanganyiko unakuwa sawia na laini.Funika dida kwa muda wa dakika 15 kwa kitambaa chepesi.
 • Kwenye ubao wa kukandia, paka unga kisha weka dida la unga. Tandaza vizuri kisha sukuma hadi uwe sawia. Kata vipande vya wastani kwa kutumia kisu kikali.
 • Funga vipande vilivyokatwa kwenye umbo la koni kisha funga kwenye ncha za koni kwa ute wa yai. Rudia hatua hii hadi vipande vya unga viishe.
 • Bandika kikaango jikoni, weka mafuta ya kula, acha yapate moto sana. Weka vipande vya koni, acha viive hadi vianze kubadilika rangi. Epua na hifadhi kwenye chombo chenye karatasi inayoweza kuchuja mafuta kisha chovya kwenye asali ya uvuguvugu.
 • Changanya matunda yaliyokaushwa (au machicha ya nazi), karanga (au korosho), maziwa na asali. Weka mchanganyiko kwenye koni kisha mwisho weka hazelnut na funga. Hifadhi pembeni na rudia hatua hii hadi umalize koni zote.
 • Unaweza kuhifadhi kwenye jokofu kwa muda na kula baadae, au unaweza kuanza kula moja kwa moja.
 • Ni vitafunwa vizuri kula kwa chai, kahawa, au kinywaji baridi. Kuwa makini, ni vitamu sana hivyo kama una matatizo na sukari usile sana.

koni-asali-misosi-poor


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.