Meatballs za viungo

Chakula hiki kinaweza kuwa mwokozi wako wakati huna kitu cha kupika. Ukiwa na mazoea ya kupika na kuhifadhi chakula vizuri kwenye fridge unakuwa na amani hata hasa wakati unapopata wageni wa ghafla na huna muda mwingi wa kufanya maandalizi kwani unaingia kwenye fridge na kuandaa chakula kizuri kwa urahisi.

Mahitaji

 • Kilo 1 ya nyama ya kusaga (Ngombe au nyama nyingine)
 • ½ kikombe cha karoti (au Karoti 4)
 • ¼ kikombe cha kitunguu maji (vitunguu 2)
 • Mayai 2
 • Limao au ndimu 1
 • Tangawizi 1
 • Kijiko 1 cha kiungo cha majani ya Italian
 • ½ kijiko cha chumvi
 • Kijiko 1 cha kitunguu saumu

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Angalizo: Hapa tunaeleza kuandaa meatballs. Ni vizuri kama utatengeneza meatballs na kuziacha kwenye fridge siku mbili au zaidi kabla hujaanza kuweka kwa mapishi ili kupata matokeo mazuri zaidi.

 • Andaa viungo vizuri kwa kukata karoti na vitunguu kwa mikono. Hakikisha ziwe nyembamba.
 • Andaa nyama yako ya kusaga kwenye chombo.
 • Changanya viungo vyote kwa pamoja. Koroga vizuri upate mchanganyiko unaofaa.
 • Baada ya muda, weka nyama kwenye viungo (unaweza kuongeza viungo unavyopenda – mie napendelea maggie, tangawizi na kunyunyuzia limao au ndimu kwa mbali).
 • Finyanga mabonge vizuri ya nyama. Unaweza kutumia kijiko ili kupata umbo zuri zaidi. Rudia zoezi hili hadi nyama iishe.
 • Weka chungu jikoni kisha weka mafuta ya kula na acha yapate moto vizuri. (Au unaweza kutumia oven kwa kuiacha ipate joto hadi nyuzi 350°C kabla ya kuanza mapishi).
 • Chungu kikiwa tayari, weka meatballs na pika hazi ziive vizuri (au kama unatumia oven, acha kwenye oven kwa muda wa dakika 30 kwenye joto la 350°C). Hakikisha meatballs zimeiva wa kuangalia kama hazina rangi ya pink kwa ndani. Endelea kupika kwa dakika 5 kama bado hazijaiva.
 • Rudia hadi umalize zoezi la kupika meatballs zote. Ukimaliza, weka kwenye mfuko wa nylon na ziweke kwenye fridge au freezer (sehemu yenye barafu) na uache kwa muda wa siku 2 ai zaidi (Itakuwa vizuri sana kama itakaa wiki au mwezi) kabla ya kuanza kupika.

Unaweza kupika hizi meatballs kwa kuandaa pasta, tomato sauce na viungo vingine unavyopendelea.


MAPISHI YAPENDWAYO

Kamba wenye mboga za majani
dakika 15
Walaji: 2

Mapishi ya ndegu kwa watoto
dakika 60
Walaji: 1

Dagaa wa nazi na karanga
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.