Kuku mwenye viungo na mbogamboga

Mimi niliandaa mapishi haya kwa kutumia kuku wa kienyeji. Kuku wa kienyeji anahitaji uvumilivu ili aive vizuri. Mie nilipunguza muda wa mapishi kwa kumpika kwenye pressure cooker. Unaweza pia kumpika kwenye sufuria ya kawaida ingawa atatumia muda kuiva.

Mahitaji

 • Kuku nusu
 • Vitunguu maji 2
 • Kitunguu saumu 1 kikubwa
 • Kolimaua au kama una mboga mboga zingine
 • Majani ya giligilani kiasi
 • Majani ya Oregano kiasi
 • Cayenne pepper kijiko 1 cha chai
 • Curry powder kijiko 1 cha chai
 • Pilipili hoho 1
 • Chumvi kiasi
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai
 • Ndimu 2
 • Mafuta kiasi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa kuku - safisha, kata vipande kisha weka kwenye chombo cha kupikia (sufuria au pressure cooker kama unatumia). Weka chumvi na ndimu. Bandika jikoni, funika vizuri. Acha nyama iive vizuri kisha epua hifadhi pembeni.
 •  Kwenye sufuria tofauti - weka mafuta ya kula, bandika jikoni. Yakipata moto weka kitunguu maji, kitunguu saumu na pilipili hoho. Usiache kukoroga ili vitunguu saumu visigande kwenye sufuria, takribani dakika 4.
 •  Weka kuku kwenye sufuria yenye mboga mboga. Koroga mpaka kuku aanze kuwa rangi ya kahawia kwa mbali. Weka kolimaua au mboga mboga za aina nyingine utalazopenda. Endelea kukoroga taratibu.
 • Weka currypowder, pilipili manga na cayyene pepper. Endelea kukoroga kama dakika 10 ili viungo vichanganyike vizuri na kuku.
 • Kamulia kipande kimoja cha ndimu, kisha weka maji kikombe 1 cha kahawa, funika.
 • Weka majani ya giligilani na oregano, koroga dakika 3 kisha epua. Ujirambe

misosi-kuku-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Macaroni ya bilinganya na nazi
dakika 15
Walaji: 2

Kachori tamu zenye giligilani
dakika 20
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.