Kuku wa broccoli

Je unafahamu kuwa broccoli ina virutubisho vingi muhimu unavyohitaji mwilini mwako ? Basi mlo huu unakula si ladha tu peke yake, bali virutubisho vyote muhimu kwa mwili wako kunawiri. Ni mlo mzuri kwa wale wasiopenda kula na kushiba sana.

Mahitaji

 • Mapaja 4 ya kuku (Tumia idadi unayohitaji kukidhi mahitaji yako)
 • Maggi cube
 • Chumvi
 • Kitunguu saumu 1 (Menya, kisha saga kiwe laini au tumia cha unga)
 • Mafuta ya kula (Nimetumia olive oil, ila unaweza kutumia pia mafuta mengine yanayotokana na mimea au samaki)
 • Broccoli (Angalia kiasi kinachotosha)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Hiki ni chakula kizuri chenye afya na kinafaa kuliwa kwa milo ya jioni isiyohitaji kushiba sana kwa afya.

Kuandaa kuku

 • Andaa kuku kwa kufuata maelezo yaliyowekwa kwenye post hii hapa.

Kuandaa Broccoli

 • Broccoli inaweza kupikwa kwa mapishi tofauti, hapa tunaangalia njia ya kupika kwa kutumia mvuke. Fuatilia maelezo kwenye picha hapo chini.
 • Osha na kisha kata broccoli kwenye vishina vyake na ubaki na broccoli zenye vifungu vichache.
 • Weka broccoli kwenye chombo unachoweza kupikia kwa mvuke. Nyunyizia chumvi kiasi na weka kwenye jiko ili mvuke upate kuivisha.
Kama una rice cooker ni rahisi kutumia kile chombo chenye matundu, ni maalum kwa mapishi kama haya.
 • Acha broccoli ipate mvuke kwa muda wa dakika 3 hadi 5. Kisha itoe.
 • Changanya brocolli na mboga nyingine za majani ulizoandaa na kisha acha ikae jikoni kwa dakika 3 hadi 4 ili zipate kuchanganyika vizuri.
 • Baada ya muda mboga yako itakuwa tayari. Jirambe.

broccoli-cook

Maelezo ya picha:

1. Safisha broccoli na maji ya bomba, au yeyote lakini yasiyotuwama

2. Kata mzizi mkuu

3. Tenganisha maua yawe pekee

4. Weka maji kwenye sufuria

5. Kwenye chujio, au chombo cha kupikia kwa mvuke, weka broccoli. Washa jiko na pika kwa dakika 4 hadi 5

6. Epua na angalia broccoli kama ni laini

7. Tenga na ujirambe

Faida za broccoli ni :

 • Kuondoa uchafu mwilini
 • Kukukinga na saratani
 • Broccoli ina virutubisho vingi muhimu unavyohitaji mwilini

MAPISHI YAPENDWAYO

Tembele
dakika 10
Walaji: 4

Mishikaki ya kupaka
dakika 45
Walaji: 3

Chicken fried rice
dakika 10
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.