Kuku wa kukaanga wa ndimu

Kuku mwenye ndimu, atakusaidia ule sana mana ile ndimu inakupa hamu ya kuendelea kula na ni mtamu sana. Unaweza kula muda wowote na kwa chakula chochote au ukaamua kula kuku mwenyewe.

Mahitaji

 • Kuku nusu
 • Ndimu 4
 • Tangawizi
 • Soy sauce
 • Paprika kijiko 1
 • Butter kikombe kimoja
 • Pilipili manga
 • Cayenne paper
 • Chumvi
 • Achali ya ndimu
 • Vitunguu saumu vilivyosagwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Weka kuku kwenye bakuli, changanya na ndimu, tangawizi, vitunguu saumu. Changanya vizuri kwa mikono safi.
 • Weka soy sauce , paprika, pilipili manga, cayenne pepper na chumvi,vichanganye vizuri kwa pamoja.
 • Chukua achali ya ndimu toa mbegu zote. Saga achali ya ndimu kisha mwagia mchanyiko kwenye kuku na changanya vizuri.
 • Weka mchanganyiko kwenye mfuko wa plastic kisha weka kwenye jokofu kwa dakika 60.
 • Weka kikaango jikoni, weka mafuta ya kukaangia (butter) subiri yapate moto. Yakipata moto,weka kuku geuza hadi waive vizuri na kua rangi ya kahawia.
 • Hapo kuku watakua tayari ruksa kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Meat loaf
dakika 60
Walaji: 4

Mapishi ya nundu
dakika 15
Walaji: 3

Kuku wa kuoka
dakika 120
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.