Kuku wa kunata mwenye sauce ya tangawizi na asali

Je wewe unahitaji nini zaidi kwenye chakula? Harufu, ladha, mvuto au? Basi, chochote unachohitaji kinapatikana kwenye huu msosi. Hii nyama inapikwa kwa muda mfupi sana, lakini matokeo yake ni mazuri mno. Ni chakula muafaka kuandaa wakati wa wikiendi kama huu ili uweze kuondoa msongo wa mazawo na uchovu wa wiki nzima. Wape uwapendao ladha tamu isiyo na mfano.

Mahitaji

 • Minofu ya kuku ½ kilo (Unaweza kuandaa kiasi kinachokutosha)
 • Asali vijiko 4 vikubwa
 • Sukari ya brown kijiko 1 na nusu vikubwa
 • Soy sauce nusu kikombe, (Ni sawa na vijiko 8 vikubwa)
 • Tangawizi iliyosagwa vijiko 2 vidogo
 • Kitunguu saumu kilichopondwa vijiko 2 vidogo
 • Chilli sauce vijiko 3 vikubwa
 • Chumvi ½ kijiko kidogo
 • Cayenne pepper kiasi
 • Mafuta ya kula, tumia mafuta ya zaituni (olive oil) vijiko 5 vikubwa
 • Currypowder kijiko 1 cha chai
 • Coriander powder kijiko 1 cha chai
 • Ndimu 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Je wafahamu kuwa chakula ni dawa pekee ya kukuweza kukusaidia kujiliwaza vizuri kuliko kitu kingine chochote? Wengi husema chakula ndio mlango wa roho, lakini pia chakula ni dawa mbadala yenye kuupa mwili furaha na nguvu. Hiki chakula ndio haswa kinachoweza kukutuliza na kukuliwaza. Kuna viungo, virutubisho na kila aina ya utamu unaohitaji. Kazi kwako.

sweet-sticky-chicken-1

 • Kwenye bakuli safi, changanya pamoja sukari, asali, soy sauce, tangawizi, kitunguu saumu, currypowder, coriander powder na chilli sauce. Koroga hadi vichanganyike vizuri. Hifadhi mchanganyiko pembeni.
 • Andaa kuku - safisha minofu ya kuku, kausha maji, kata vipande vidogo kisha hifadhi kwenye chombo safi. Nyunyizia chumvi, cayenne pepper na ndimu kiasi kisha changanya ili vipate kuenea vizuri.

Hakikisha kuwa ni minofu na imekatwa vipande vyembamba na vidogo ili viive vizuri na haraka. Hii ndio swala la msingi kwenye haya mapishi.

 • Bandika kikaango jikoni, hakikisha moto uwe mkali sana. Weka mafuta ya kula kiasi kidogo sana, kama kijiko kimoja hivi kikubwa. Mafuta yakipata moto weka minofu ya kuku. Weka nyama kiasi tu ili upate nafasi ya kugeuza na kuipa nafasi nyama iive vizuri. Acha upande mmoja uive vizuri kwa muda wa dakika 1 hadi 2 kisha geuza upande wa pili – hakikisha nyama haiungui. Upande wa pili ukishaiva toa nyama weka pembeni. Rudia kwa nyama iliyobaki hadi umalize.
 • Awamu ya mwisho ya nyama ikishaiva, usitoe kwenye kikaango, bali chukua nyama iliyokwishaiva weka kwenye kikaango. Geuza kwa pamoja kisha mwagia sauce uliyoandaa. Koroga vizuri ili sauce ichanganyike na nyama. Hakikisha huachi kukoroga hadi sauce iwe inanata na imekuwa nzito. Hapo kuku wako atakuwa tayari. Epua na tenga chakula.
 • Hii mboga inaweza kuliwa yenyewe au na chakula kama wali, ugali, viazi, au na vitafunwa tofauti. Jirambe na ladha ya maisha.

sweet-sticky-chicken-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi na nyama ya kusaga
dakika 25
Walaji: 2

Chachandu ya embe
dakika 15
Walaji: 4

Bagia za kunde
dakika 7
Walaji: 4

Maandazi ya Vanila na Nazi
saa 1
Walaji: 15

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.