Kuku wa kuoka

Kuku wa kuoka ni mtamu na utafurahia ladha yake pamoja na familia yako. Unaweza kula aina hii ya kuku kwa chips, ugali, ndizi za kuchoma au chakula chochote kile unachopendelea. Ni nzuri pia kushushia na kinywaji murua ili kuona ladha na utamu wa nyama ya kuoka.

Mahitaji

 • Kuku (usikate vipande)
 • Butter
 • Chumvi
 • Pilipili manga
 • Thyme
 • Majani ya rosemary
 • Foil paper
 • Curry powder

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Washa oven na acha ipate joto hadi nyuzi 325°F.
 • Weka kuku kwenye sinia (frying pan) ya kuokea - au chombo mahsusi kinachoingia kwenye oven.
 • Paka butter juu ya kuku hadi ienee vizuri.
 • Paka curry powder kwa ndani ya kuku. Curry ni mchanganganyiko wa viungo vingi tofauti, hivyo ni mahsusi kuleta ladha tamu na harufu nzuri.
 • Nyunyizia chumvi kisha sambaza kwa ndani na nje vizuri.
 • Paka pilipili manga ya kutosha juu ya kuku.
 • Nyunyizia limao la kutosha, kisha weka majani ya thyme na rosemary yaliyosagwa.
 • Funga nyama ya kuku kwenye foil paper kisha weka kwenye oven. Tega oven yako kwa muda wa saa nzima na dakika 20. Huu ni muda mzuri kwa kuku kuiva vizuri nje na ndani.
 • Baada ya muda kuisha angalia kama kuku ameiva vizuri
  Unaweza kupima nyama kama imeiva kwa kutumia kipimajoto (thermometer), ambayo ni maalumu kwa nyama au pia unaweza kukata kipande kidogo na kuangalia kama nyama imeiva vizuri.
 • Nyama ikiiva, toa kuku. Weka pembeni ili ipoe kwa takribani dakika 20.
 • Nyama ya kuku itakuwa tayari kuliwa. Jirambe na ladha ya maisha.

MAPISHI YAPENDWAYO

Meat loaf
dakika 60
Walaji: 4

Mapishi ya nundu
dakika 15
Walaji: 3

Kuku wa kuoka
dakika 120
Walaji: 5

Nguru wa kuchoma
dakika 40
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.