Kuku wa kuoka na ndizi mzuzu

Utamu wa hiki chakula utaujua baada ya kukila, si wa kuhadithiwa. Kwa ufupi, ni chakula rahisi kuandaa na kina afya inayotakiwa. Ni vizuri kukipika kama una muda kiasi, lakini ladha utakayoipata huwezi kuelezea

Mahitaji

 • Kuku mapaja 4
 • Ndizi mzuzu4
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Cube maggie 1
 • Olive oil
 • Limao 1
 • Kitunguu maji 1
 • Pilipili hoho nyekundu 1, ya kijani 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Tunapika chakula cha kuku, ambaye ataonekana kama hivi akishaiva

pic00

Karibu sana kujumuika nasi.

1. Andaa kuku

 • Osha na kisha chanja ngozi kiasi. Weka kuku kwenye bakuli au chombo kinachoingia kwenye oven. Weka chumvi na limao kisha changanya vizuri. Hakikisha unapaka viungo ndani ya kuku, yaani kati ya ngozi na nyama.  Usitoe ngozi ili kuku aive vizuri kwenye oven bila kuungua.

pic2

 • Weka cube maggie, changanya vizuri. Hakikisha mchanganyiko unaingia vizuri kwenye nyama ya kuku.
 • Weka kitunguu saumu kilichopondwa kwenye kuku. Paka vizuri juu ya  nyama na juu ya ngozi.
 • Unaweza kuacha kuku na viungo kwa muda wa dakika 20 hadi 30 ili viungo vipate kuingia vizuri. Wakati huo unaendelea kuandaa viungo vingine.

2. Andaa viungo wakati kuku anachanganyika na viungo:

 • Kata pilipili hoho na kisha tenga kwenye chombo pembeni.
 • Menya kisha kata kitunguu maji na karoti kwenye vipande vidogo kisha hifadhi kwenye chombo.
 • Menya ndizi, kata vipande vidogo na hifadhi kwenye chombo pembeni.

Unaweza kuweka chumvi kidogo lakini si muhimu maana viungo vingi vina chumvi.

pic0

3. Baada ya dakika 20 hadi 30

 • Washa oven ili ipate moto kabla hujaanza kuoka kuku. Weka kwenye nyuzijoto 250°C.
 • Changanya viungo vilivyobaki pamoja na kiwango kidogo cha ndizi kwenye bakuli lenye kuku.
 • Nyunzizia mafuta ya olive juu ya nyama. Mafuta husaidia kuivisha nyama na kuifanya isikauke.
 • Unaweza kukoroga kiasi ili upate mchanganyiko sawia lakini si lazima sana.

pic5

 • Weka bakuli lenye mchanganyiko wa kuku, viungo na ndizi kwenye oven. Tega muda dakika 45 hadi 60. Hakikisha unageuza mara kwa mara ili nyama iive vizuri pande zote.

pic8

4. Kaanga ndizi zilizobaki

 • Bandika kikaango jikoni. Weka mafuta ya kula ya kutosha.
 • Mafuta yakipata moto vizuri weka ndizi kiasi, kuwa makini usirundike ndizi sababu hazitaiva vizuri. Fuata ushauri huu hapa.

pic7

 • Geuza ndizi mara tu zinapobadilika rangi na kuwa brown (rangi ya udongo)
 • Ndizi zikiiva toa na weka kwenye chujio lenye karatasi kama tissue ili kunyonya mafuta vizuri. Tissue wengine wanaita paper towel.

pic9

 • Ukimaliza kupika ndizi hifadhi na usubirie nyama iive.

5. Andaa chakula

 • Kata tango na nyanya. Weka kwenye sahani
 • Weka ndizi kiasi. Unaweza kuchanganya ndizi za kwenye oven na ndizi za kukaanga.
 • Tenga kipande cha kuku. Chakula hiki kimepikwa ili kila mtu ale kipande 1, hivyo watu 4.
 • Ongeza vikorombwezo unavyopenda - pilipili, chachandu na vingine.

pic10

Angalizo: kuku wa kuoka huwa anakuwa na mchuzi, unaweza kuutumia mchuzi kama kiambato kwenye mboga za majani au kama supu. Ni nzuri maana ina virutubisho vyote na huwa ni tamu sana.

Jirambe na usisahau kutupa feedback.


MAPISHI YAPENDWAYO

Kamba wenye mboga za majani
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.