Kuku wa kuoka na sauce ya pilipili

Mapishi haya ni maalumu kwa ajili ya hii sauce ya pilipili. Ni sauce inayoweza kuliwa na kitu chochote kile na ikapendeza. Kinachonifurahisha zaidi ni ile hali ya kukufanya ujisikie hamu ya kula lakini kukushibisha mapema kutokana na ngano iliyomo ndani yake. Ni sauce nzuri sana kwa kula na vyakula

Mahitaji

 • Macaroni (Pima yanayowatosha)
 • Maziwa (si lazima sana kama hupendelei maziwa kwenye macaroni)
 • Kuku vipande 2
 • Majani ya korianda
 • Siagi (butter, mafuta ya kula mazito yale)
 • Pilipili manga (unga au mbegu)
 • Unga wa ngano 200g

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Uhondo wa hiki chakula huwezi kuhadithiwa, shurti ule na uone raha yake. Ni chakuka kizuri kwa kula sababu kinavutia na kitamu hasa, kama kinavyoonekana.

1. Andaa Macaroni

 • Chemsha Macaroni kwenye maji huku ukiongeza chumvi kiasi. Yakishaiva, weka chombo jikoni kisha pitisha kidogo kwenye mafuta ya moto ili kuyapa ladha zaidi (nimetumia siagi au butter, unaweza kutumia mafuta yeyote unayopendelea). Mwagia maziwa kiasi ili kuongeza ladha zaidi.

2. Andaa kuku

Unaweza kuandaa kuku huyu kwa njia tofauti, mfano kama hii au hii.

 • Weka viungo unavyopendelea (nimetumia maggi cube, chumvi na kituunguu saumu). Hifadhi kwa muda.
 • Baada ya muda, kaanga kwenye mafuta au oka kwenye oven. (Ni changuo lako. Kwa wale wasiopenda sana mafuta unaweza kuoka kwenye oven. Binafsi napenda kuoka zaidi)

3. Andaa sauce ya pilipili

 • Bandika kikaango, weka siagi (butter). Ikichemka, weka unga na koroga vizuri.
 • Ongeza maji, yawe kiasi kama robo kikombe, kisha endelea kukoroga.
 • Weka viungo unavyopenda. Kwenye mapishi haya niliweka mie napenda magi cube ili iwe na ladha nzuri na harufu tamu.
 • Weka pilipili manga, mie nilitumia ya unga, kisha koroga na acha ichemke kwa dakika 4 hadi 6.
 • Ukitoa sauce unaweza kuongeza pilipili. Hii sauce shurti iliwe na pilipili kali, ndo raha utaiona.
 • Jirambe na kuku mwenye pilipili ya kutosha.

MAPISHI YAPENDWAYO

Cornbread wenye zabibu kavu
dakika 40
Walaji: 3

Paella
dakika 30
Walaji: 8

Beef Rendang
dakika 60
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.