Kuku wa kuoka na tambi

Chakula kitamu, rahisi kuandaa na kinachoweza kuliwa wakati wowote ule. Jaribu mapishi haya na upate kujua ladha tamu ya maisha.

Mahitaji

 • Kuku mapaja 2
 • Ndizi mzuzu 2
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu saumu 1
 • Cube maggie 1
 • Olive oil
 • Tambi
 • Limao 1
 • Kitunguu maji 1
 • Pilipili hoho nyekundu 1, na ya kijani 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula tunachokula leo kitaonekana hivi baada ya kumaliza kuandaa:

20141201_183202

1. Andaa Kuku

Nilikuwa na hamu ya kubadilisha chakula baada ya kutokuwa na hamu. Nikakumbuka kuku wa kuoka, hivyo basi, bila kuchelewa nikaandaa mapishi haya, maana nilikuwa na hamu ya kula kuku mtamu kiasi hiki. Sasa, ili kumuandaa kuku huyu vizuri, tafadhali fuata maelekezo hapa kuhusu kuku wa kuoka maana nimempika kwa style kama mapishi niliyoweka kwanza.  

Ili kuleta vionjo vizuri mie nikala tambi, kuku pamoja na maharage. Ladha murua ya chakula hiki, harufu nzuri ya viungo na utamu wake ni murua kukupa raha ya maisha baada ya wiki ndefu ya uchovu nyumbani.

 • Andaa kuku kwa kufuata hatua hizi

Kuku atakuwa kama hivi baada ya kumaliza

pic00

2. Andaa Ndizi

 • Menya na kisha kata ndizi mzuzu vipande vidogo
 • Weka kikaangio jikoni, weka mafuta na subiria yapate moto
 • Weka ndizi jikoni, acha kwa muda ziive, kisha geuza ili zipate kuiva vizuri pande zote.
 • Hakikisha usilundike ndizi kwenye kikaangia maana hazitoiva vizuri. Weka ndizi zinazotosha ili kupata matokeo mazuri
 • Ndizi zikiiva toa na weka kwenye chombo pembeni. Rudia kwa vipande vilivyobaki hadi umalize

pic9

3. Andaa Tambi 

Ni vizuri kuandaa tambi mwisho ili kula mara tu baada ya kumaliza. Tambi zikipoa hazina ladha nzuri, hivyo ni bora kula wakati bado za moto na zina virutubisho vingi zaidi.

 • Weka sufuria jikoni, weka tambi na ongeza chumvi
 • Baada ya dakika 5 hadi 6 angalia kama tambi zimeiva, kisha toa na tenga pembeni
 • Andaa tambi pamoja na kuku na ndizi tayari kwa kujiramba.

20141201_183303

Ukiwa na swali au wazo, tafadhali tuandikie baruabebe info (at) misosi (dot) co (dot) tz au tuma maoni hapa chini na sisi tutakujibu haraka iwezekanavyo.

Asante kwa kufurahia ladha ya maisha pamoja nasi 


MAPISHI YAPENDWAYO

Beef Masala
dakika 15
Walaji: 4

Keki ya chocolate
dakika 55
Walaji: 4

Lemonade ya tangawizi
dakika 70
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.