Kuku wa mboga za majani

Kuku anaweza kupikwa kwa aina tofauti. Hii ni mojawapo ya mapishi ya kuku yanayoweza kuliwa kwa vyakula tofauti na vingi, mfano ugali, wali, ndizi, chapati, viazi, mihogo au unaweza kula yenyewe kama ilivyo na ikanoga pia.

Mahitaji

 • Minofu ya kuku ½ kilo
 • Kitunguu saumu
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Limao au ndimu 1
 • Pilipili hoho – kijani, njano na nyekundu
 • Pilipili manga
 • Curry powder
 • Tangawizi 1
 • Vitunguu maji 2
 • Olive oil

20141221_183602

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa nyama ya kuku itakayokuwa kama hivi ikishaiva

20141221_193805

 • Kata minofu ya kuku kwenye vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kuiva.

Nyama hii haichemshwi bali inaanza kukaagwa moja kwa moja, hivyo vipande vidogo vidogo vinasaidia kuifanya iive vizuri hadi ndani.

20141221_185523

 • Osha nyama vizuri. Weka kwenye chombo kikavu.
 • Nyunyuzia chumvi. Koroga.
 • Nyunyuzia limao, kisha koroga zaidi.
 • Weka tangawizi iliyopondwa ili kuipa nyama ladha nzuri. Acha nyama ikae kwa dakika 5 hadi 7 ili limao lipate kuingia.
 • Wakati nyama inakolea limao. Kata kitunguu maji kwenye vipande vidogo, kisha weka kwenye chombo pembeni.
 • Kata pilipili hoho kwenye vipande virefu kiasi. Weka kwenye chombo pembeni.
 • Kata karoti kwenye vipande vidogo. Weka kwenye chombo pembeni.

20141221_184939

 • Weka kikaangio jikoni, ongeza mafuta ya olive. Acha yapate moto kiasi

20141221_190911

 • Weka nyama jikoni. Koroga kiasi kisha acha iive vizuri hadi ianze kubadilika rangi kuwa ya rangi ya udongo.

20141221_191025

 • Weka pilipili manga juu ya nyama. Nyama ikiwa tayari ipua kisha hifadhi pembeni.

20141221_192623

 • Weka mafuta kwenye kikaangio. Subiri yapate moto kisha weka vitunguu.
 • Weka kitunguu saumu. Koroga vizuri acha viive pamoja na vitunguu maji.

20141221_193241

 • Weka pilipili hoho, koroga mchanganyiko. Baada ya dakika moja weka karoti na endelea kukoroga. Acha viive kwa dakika 3 hadi 5.

20141221_193355

 • Weka nyama ya kuku iliyoiva kwenye mchanganyiko wa mboga za majani.
 • Ongeza curry powder, koroga mchanganyiko vizuri. Funika na mfuniko. Acha ichemke vizuri. Takribani dakika 5 hadi 7.

20141221_193526

 • Ipua mboga yako na iko tayari kuliwa

Unaweza kula na wali, ugali, ndizi, viazi, chapati na vinginevyo vingi. Chaguo ni lako.


MAPISHI YAPENDWAYO

Cutlets za pilipili
dakika 5
Walaji: 4

Wali wenye nazi na maziwa
dakika 20
Walaji: 2

Nyama tamu yenye pilipili
dakika 25
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.