Kuku wa mchuzi

Kuku ni mtamu, lakini kwa mapishi kama haya utamu unakuwa maradufu. Ni chakula kitamu, kizuri na chenye ladha ya kipekee. Kuku aliyekaangwa na kisha kuwekwa rojo ya mchuzi anazidi utamu maradufu ya yule wa kuchemsha moja kwa moja. Ili kuelewa utamu wake, jaribu pishi hili.

Mahitaji

 • Vipande vya kuku (Unaweza kuwa na idadi yeyote, kutegemea na walaji)
 • Mafuta ya kukaangia (Vizuri kama ukiwa na mafuta yanayotokana na mimea)
 • Chumvi
 • Pilipili manga
 • Kitunguu saumu cha unga
 • Tangawizi ya unga kijiko 1 cha chai
 • Limao 1
 • Pilipili hoho 2
 • Kitunguu maji 1
 • Karoti 2
 • Nyanya au tomato paste
 • Royco, maggie au chochote unachopenda kuweka kwa kuleta ladha

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kwa kawaida imezoleka kuanza chemsha kuku, halafu tunamkaanga. Hata mie huwa nafanya hivyo. Lakini leo tutatengeneza hiki chakula tofauti kidogo. Tutaanza kukaanga kuku halafu tutakuja kuwapika kwenye mchuzi mzito wa nyanya na mboga mboga. Ladha tamu ya viungo na kuku vinafanya hii supu kuwa maridadi na raha kabisa kuila kwa mchuzi. 

20150124_220609

 • Andaa kuku, kata kwenye vipande unavyoweza kula, osha vizuri na weka pembeni. Usiwatoe ngozi, ili isaidie kuiva vizuri. Ngozi huiva vizuri wakati wa kukaanga.
 • Weka viungo kwenye kuku – limao, chumvi, kitunguu saumu, tangawizi, na pilipili manga. Acha viungo viingie vizuri kwa muda wa dakika 15 hadi 20. Unaweza kuacha zaidi ili nyama ipate kuingia vizuri, lakini si lazima sana.

20150124_203013

 • Weka mafuta jikoni kwenye chombo kinachotosha. Acha yapate moto vizuri, kisha weka vipande vya kuku.

20150124_204053

 • Acha kuku waive vizuri hadi wakauke na kubadilika rangi. Inachukua kama dakika 10 hivi. Toa kuku na weka kwenye tissue paper, ili wachuje mafuta vizuri. Rudia hatua hii kwa vipande vilivyobaki.

20150124_205750

 • Andaa nyanya (au kama una tomato paste ni vizuri zaidi), pilipili hoho na karoti wakati kuku anaendelea kukaangika vizuri.
 • Kuku akishaiva, bandika kikaangio au sufuria jikoni. Weka mafuta ya kula kiasi, acha yapate moto.
 • Weka kitunguu, acha kiive na kilainike. Weka nyanya, koroga na acha ichemke kiasi hadi zilainike. Weka karoti, na pilipili hoho. Funika acha zipate kuiva kiasi.
 • Weka vipande vya kuku unavyotaka kuvipika. Koroga vizuri. Ongeza Maggie, au royco mchuzi mix ili upate kuleta ladha zaidi. Koroga vizuri.
 • Acha kati ya dakika 5 hadi 10 ili vipate kuivia na kuleta ladha nzuri.

20150124_213856

 • Ukimaliza unaweza kutoa na kuacha ipoe au ukala moja kwa moja na chakula chako – ugali, wali, mkate, au hata maandazi. Ni chaguo lako.
 • Jirambe na kuku wako. Mie huwa napenda kuweka na vipande vya kuku wa kukaanga, hivyo hapa nimechanganya, ila ni uamuzi wako, maana kuchanganya utamu ndio unanoga zaidi.

20150124_220827

20150124_220717

20150124_220732

 


MAPISHI YAPENDWAYO

Kachori tamu zenye giligilani
dakika 20
Walaji: 6

Keki tamu ya mtindi na vanilla
dakika 50
Walaji: 8

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.