Kuku wa limao

Hiki ni chakula kizuri kuandaa muda ulio na familia na kula pamoja, mida ya jioni au wakati wa vikao weekend. Ni chakula kizuri sababu ni kitamu na kimeandaliwa na viungo bora, hivyo kina afya tele. Hakikisha tu unafanya zoezi mara kwa mara

Mahitaji

 • Kuku 1
 • Mafuta ya kula (mie nimetumia mafuta ya mizeituni au Olive oil)
 • Kikombe 1 cha kahawa
 • Kitunguu saumu cha unga vijiko 3 vya chakula
 • Malimao 4
 • Paprika nusu kijiko cha chai
 • Unga wa kitunguu saumu kijiko 1 cha chai
 • Vitunguu maji 2 vikubwa
 • Chumvi kijiko 1 na nusu cha chai
 •  Pilipili manga kijiko 1 cha chakula
 • Maji kikombe kidogo (ukubwa wa kikombe cha kahawa)
 • Kijiko 1 kidogo cha Unga wa haradali (Mustard powder)
 • ½ kijiko cha chai cha thyme
 • ½ kijiko cha chai cha lemon zest (Hupatikana kwenye maduka ya vyakula).

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Huyu kuku ni mtamu, na ni chakula bora sana kwa familia. Kama unahitaji kujiramba na kuvinjari, basi hapa ndio umefika. Ila, hakikisha tu unafanya zoezi mara kwa mara , maana huyu kuku lazima utavimbiwa.

citrus-grilled-chicken

 • Changanya viungo (kasoro mafuta ya kula na ndimu) kwenye blender. Saga ili upate mchanganyiko sawia. HIfadhi pembeni.
 • Andaa kuku – unaweza kumkata vipande au ukamuacha mzima kasha msafishe na mkaushe kwa kitambaa safi.

Kama unataka kuoka kuku, hakikisha kuwa huondoi ngozi. Ngozi husaidia kumfanya kuku aive vizuri sababu inaungua huku ikiacha nyama ya ndani ikiiva vizuri na taratibu.

 • Kwenye mfuko wa nylon au plastic (au hata bakuli kama huna mfuko) weka mchanganyiko wa viungo vyote kisha weka kuku na umchanganye vizuri ili apate kuingia viungo.

citrus-marinated-chicken-3-

 • Hifadhi mfuko wenye kuku kwenye fridge kwa takribani masaa 6 hadi 7 (ila ni vizuri kama ukiacha usiku mzima ili vipikwe kesho yake)
 • Ukiwa tayari kuandaa kuku, toa kwenye mfuko, panga kwenye bakuli (sinia au chombo chochote) la kuokea kwenye oven.
 • Washa oven na uipashe moto kwenye nyuzi 300°F (150°C)
 • Kamua limao kwenye chombo kikavu. Changanya maji ya limao na mafuta ya kula (mfano, olive oil) kwa pamoja upate mchanganyiko sawia. Kata vizuri vipande vya limao lililobaki na weka pembeni, usitupe.
 • Mwaga mchanganyiko juu ya vipande vya kuku vizuri. Mloanishe ili apate kuwa na unyevunyevu mzuri.
 • Panga vipande vya limao kwenye bakuli vizuri pembeni ya vipande vya kuku.
 • Tega oven kwa dakika 45 na weka kuku ili apate kuiva. Unaweza kuangalia kama anaungua ili kumgeuza.

citrus-marinated-chicken-5-

 • Baada ya dakika 45, toa kuku. Angalia kama ameiva vizuri ndani.
 • Unaweza kula chakula hiki na ugali, wali, ndizi au vinginevyo. Unaweza pia kula kama kitafunwa kizuri na kinywaji baridi.
 • Jirambe, maana huyu kuku ni mtamu.

MAPISHI YAPENDWAYO

Samaki wa kukaanga
dakika 15
Walaji: 4

Viazi vya mayai na kamba
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.