Kuku wa viungo na viazi vya kuoka

Hiki ni chakula ni kitamu na bora. Utamu wake unatokana na uwepo wa viungo vizuri vilivyochanganywa na kuku. Ubora wake unatokana na uwepo wa viazi vilivyo na maganda. Maganda ya viazi yana kiwango kikubwa cha madini ya chuma, hivyo kukifanya chakula hiki kuwa kizuri kwa wale wanaohitaji madini ya chuma kwa wingi. Ni chakula chepesi kinachokupa shibe ya kukutosha muda mrefu.

Mahitaji

 • Mapaja ya kuku 4
 • Curry powder kijiko 1
 • Tangawizi ya unga kijiko 1
 • Pilipili nyekundu ya unga kijiko 1
 • Chumvi kijiko ½ kijiko
 • Chicken cube 1
 • Limao 1
 • Ufuta vijiko 2
 • Mafuta ya kula vijiko 3
 • Chicken Tandoori kijiko 1
 • Viazi mbatata 8

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 Wakati unaandaa hiki chakula jaribu pia kuandaa chachandu au kachumbari ya kula pamoja nacho. Uwepo wa pilipili hukifanya hiki chakula kunoga na kuwa na ladha murua zaidi.

 • Andaa kuku – osha na safisha vizuri, usitoe ngozi. Nyunyia chumvi, changanya vizuri na kisha mwagia limao. Paka nusu kipande cha limao vizuri kwenye kuku – hakikisha limeingia kati ya ngozi na nyama ya kuku. Hifadhi pembeni kwa dakika chache.
 • Kwenye bakuli, changanya  viungo vyote vilivyobaki vya kuku – chicken curry, tandoori, tangawizi na pilipili nyekundu. Koroga vizuri. Ikishakuwa safi, kamulia nusu ya kipande cha limao. Changanya vizuri.
 • Paka mchanganyiko wa viungo kwenye mapaja ya kuku vizuri. Hakikisha mchanganyiko umeingia vizuri. Hifadhi nyama kwenye jokofu kwa muda wa dakika 40 hadi 50 ili viungo vipate kuchanganyika vizuri na nyama.
 • Ukiwa tayari kupika, paka mafuta ya kula kwenye mapaja ya kuku kisha nyunyizia ufuta juu ya kuku. Mafuta yanalainisha nama na kuifanya isikauke au kuungua wakati wa kuoka. Washa oven, weka kwenye nyuzi 200°C (392°F) acha ipate moto kwa muda.
 • Osha viazi vizuri. Usimenye. Paka mafuta kiasi juu ya ngozi ili vipate kuiva vizuri, paka chumvi kwenye viazi. Panga viazi na nyama kwenye waya wa kuchomea kwenye oven. Weka kwenye oven.  Tega muda wa dakika 50 na acha viive vizuri.
 • Baada ya muda  kupita, toa kwenye oven na tenga ujirambe.

misosi-kuku-viazi-two


MAPISHI YAPENDWAYO

Sambusa za nyama
dakika 15
Walaji: 10

Macaroni ya cheese
dakika 20
Walaji: 3

Peanut butter cookies
dakika 10
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.