Lasagna

Lasagna ni chakula asili ya kiitaliano (Italian dish) ambacho huandaliwa kwa kuwekwa matabaka (layers) ya sauce ya nyama, cheese, noodles (tambi) na pasta. Mapishi haya ya lasagna ni bora kuandaa na kula na familia, hasa wakati wa weekend maana utakuwa na muda mzuri wa kuandaa na kuyapa ladha tamu.

Mahitaji

 • ½ Kilo ya Italian sausage
 • ¼ kilo ya nyama ya ng’ombe ya kusaga
 • ½ kikombe cha vitunguu maji vilivyokatwa
 • Punje 2 za kitunguu saumu, zilizopondwa
 • Nyanya ya kopo (Totamo paste) makopo 2 madogo (vikombe 2)
 • Nyanya 4 zilizomenywa na kusagwa
 • Tomato sauce kikombe 1
 • ½  kikombe cha maji
 • Vijiko 2 vya sukari nyeupe
 • Kijiko 1 ½ cha chai cha majani makavu ya basil
 • ½ kijiko cha chai cha mbegu za fennel
 • Kijiko 1 kikubwa cha chumvi
 • ¼ kijiko cha pilipili manga ya unga
 • Vijiko 4 vikubwa vya majani ya parsley yaliyokatwa vipande
 • Tambi za lasagna (Lasagna noodles) 12 (zinakuwa pana)
 • ½  kilo ya ricotta cheese
 • Yai 1
 • Chumvi ½  kijiko cha chai
 • ¼ kilo ya mozzarella cheese, kata vipande
 • ¾ kikombe cha Parmesan cheese iliyokwanguliwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Mapishi haya yanatumia viungo vingi, lakini matokeo yake ni chakula kitamu kinacholiwaza roho za walaji. Jaribu na utupe majibu yake.

misosi-lasagna-web

 • Kwenye sufuria, andaa sauce ya nyama mchanganyiko . Weka mafuta kiasi, yakipata moto weka Italian sausages, ponda ili zilainike vizuri, koroga mara kwa mara ili ziive vizuri. Weka nyama ya kusaga, koroga vizuri. Weka kitunguu maji, na kitunguu saumu. Joto liwe la wastani hadi nyama inapogeuka kuwa brown.
 • Weka nyanya zilizosagwa, nyanya ya kopo, tomato sauce na maji. Koroga. Ongeza sukari, basil, mbegu za fennel, kijiko 1 kikubwa cha chumvi, pilipili, na vijiko 2 vikubwa vya parsley. Pika kwenye moto wa wastani, funika kwa saa 1½, huku ukiwa unakoroga mara kwa mara kuweka joto sawa kwenye mboga yote.
 • Bandika sufuria tofauti jikoni yenye maji na chumvi. Acha maji yachemke vizuri. Pika tambi za lasagna (lasagna noodles) kwenye maji ya moto kwa dakika 8 hadi 10 (Vizuri ukipika chini ya muda ulioshauriwa ili ziive vizuri). Toa noodles, chuja maji ya moto na zichovye kwenye maji ya baridi ili sizigandiane.
 • Kwenye bakuli kubwa, changanya ricotta cheese na yai, parsley zilizobaki na ½  kijiko cha chai cha chumvi.
 • Washa oven kwenye nyuzijoto 375 °F (190 °C). Acha ipate moto kwa dakika 5 hadi 7.
 • Anza kupanga lasagna kwenye bakuli ya kuokea. Tandaza kikombe 1½ cha sauce ya mchanganyiko wa nyama kwenye chombo cha kuokea.  Panga noodles 6 kwa urefu, huku zikipandiana kidogo kwa upande, juu ya sauce ya nyama hadi ufunike sauce ya nyama. Tandaza nusu ya mchanganyiko wa ricotta cheese juu ya noodle na kisha weka vipande vya jibini ya mozzarella (mozzarella cheese) juu yake. Rudia kwa kuweka tena kikombe 1½  cha sauce ya nyama juu ya jibini ya mozzarella (mozzarella cheese) na kisha nyunyizia ¼ kikombe cha Parmesan cheese. Rudia haya matabaka kwa kujazia na mozzarella cheese hadi sauce yako inapoisha au bakuli ya kuokea (au chombo cha kuokea) ikijaa.
 • Funika bakuli (au chombo cha kuokea) na foil paper. Ili kuepuka foil paper kugandia lasagna kunyunyizia oil inayozuia kuganda au hakikisha foil paper haigusi cheese na mchanganyiko ulio kwenye bakuli.
 • Weka bakuli ya kuokea kwenye oven. Oka kwa dakika 25 kisha toa foil paper na oka tena kwa dakika 25 zaidi. Toa na acha ipoe kwa dakika 15 kabla ya kutenga na kula.
 • Jirambe na pishi bora la lasagna.

misosi-lasagna-0


MAPISHI YAPENDWAYO

Mkate wa boga
dakika 60
Walaji: 5

Njegere za nazi na maziwa
dakika 35
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.