Lemonade ya tangawizi

Kinywaji hiki ni rahisi kuandaa na ni kizuri kwa afya zetu. Uwepo wa limao na tangawizi unasaidia mwili kupata virutubisho na vitamini mbalimbali mwilini. Epuka kutumia sukari nyingi mana si nzuri kwa afya. Mi niketumia asali kiasi.

Mahitaji

  • Malimao fresh 6
  • Asali kikombe 1
  • Tangawizi iliyokwanguliwa nusu kikombe
  • Maji vikombe 2
  • Maji ua baridi vikombe 14

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

  • Chukua bakuli safi, kwenye bakuli kamua malimao kisha toa mbegu zote, yabaki maji ya limao.
  • Washa jiko, bandika sufuria weka vikombe 2 vya maji, asali na tangawizi. Acha mchanganyiko uchemke kwa moto mdogo kwa muda wa dakika 10, mpaka asali iyeyuke na harufu nzuri ya tangawizi isikike.
  • Epua, acha ipoe. Chukua jagi safi. Kwenye jagi, weka maji ua limao, maji ya baridi vikombe 14 kisha weka mchanganyiko ulioutoa jikoni. Changanyanya vizuri weka kwenye jokofu kwa muda wa lisaa limoja. Kama utapenda weka majani ya mnanaa na giligilani ili kupata harufu nzuri. 
  • Jirambe

MAPISHI YAPENDWAYO

Mishikaki ya kupaka
dakika 30
Walaji: 4

Ugali wa muhogo na mlenda
dakika 15
Walaji: 2

Koliflawa na nyama ya kusaga
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.