Lishe ya mtoto yenye viazi ulaya, kuku, carrot na sweetcorn

Chakula hiki ni kizuri kwa watoto wote ila ni vizuri kuanzia mtoto wa miezi 9 na kuendelea. Ni kitamu na mtoto atakifurahia. Usimpe mtoto chini ya miezi mana mchanganyiko huu ni mkubwa sana kwa watoto chini ya miezi 9.

Mahitaji

 • Butter yenye chumvi 25g
  Kitunguu maji 1
  Karoti 3
  Viazi ulaya robo kg
  Sweetcorn 50g
  Maziwa robo lita yaliyochemsha kabisa
  Kuku aliyechemshwa na asiye na ngozi wala mifupa robo kg
  Supu ya kuku kikombe 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Washa moto, bandika sufuria jikoni.
  Weka butter ikiyeyuka na kuchemcha, weka kitunguu maji, koroga kwa dakika 1, weka karoti endelea kukoroga kwa dakika 5.
  Weka viazi na kuku ( mkate vipande vidogo sana) endelea kukoroga kwa muda, ongeza mchuzi.
  Funika vizuri mvuke usitoke, funika kwa dakika 15.
  Weka sweetcorn, ziache kwa dakika 10. Kisha epua acha zipoe.
  Weka kwenye brenda, ongeza maziwa kisha saga. Muekee mtoto ajirambe.
  Kikibaki hifadhi kwenye jokofu (freezer), kinaweza kutumika wiki 4 usizidishe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Wali & mboga mseto
dakika 45
Walaji: 4

Pilau la basmati
dakika 35
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.