Maandazi ya apple

Jinsi ya kuandaa vitafunio vyepesi, rahisi na visivyochukua muda mrefu. Maandazi haya ya apple ni matamu na kitafunwa kizuri kwa familia. Unaweza kuandaa na kuhifadhi vizuri kwenye jokofu na kula unapopendelea. Ili kuweza kuyahifadhi vizuri funga kwenye karatasi laini za kuhifadhia chakula kabla ya kuweka kwenye jokofu.

Mahitaji

 • Unga wa ngano 250 g
 • Hamira kijiko 1
 • Mayai 2
 • Maziwa ½ kikombe
 • Apple 4
 • Chumvi ½ kijiko
 • Mafuta ya kula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kwenye bakuli, weka unga na hamira kisha changanya vizuri. Pasua mayai, chuja kiini na ute. Weka viini kwenye unga pamoja na sukari kidogo. Changanya pamoja vizuri.
 • Weka maziwa kwa awamu huku unaendelea kuchanganya unga. Dida likiwa na uzito ulio wastani weka ute wa yai, uwe umekorogwa vizuri.
 • Menya apples, kisha kata kwenye vipande vya uviringo vya wastani vilivyo sawa. Chovya vipande kwenye dida vinyonye dida kwa juu.
 • Bandika mafuta jikoni, acha yapate moto vizuri. Yakishapata moto weka vipande vya apple, acha viive kwa dakika 3 hadi 5. Kisha toa na weka pembeni kwenye chombo kisafi.
 • Rudia hatua hii hadi vipande vyote vya apple na dida viishe.
 • Unaweza kuweka sukari na coating tofauti za icing sugar kwenye haya maandazi ili kukupa ladha.
 • Unaweza kula maandazi haya upendavyo – kwa chai, kawaha, maziwa, au kwa kulumagia. Jirambe.

maandazi-misosi-misosi-high


MAPISHI YAPENDWAYO

Mkate wa kiwavi wenye kuku
dakika 40
Walaji: 6

Kuku wa mchuzi
dakika 25
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.