Maandazi ya Vanila na Nazi

Maandazi ni kitafunwa ambacho ni kitamu na laini kinavutia machoni. Unaweza kula kwa kunywa na chai, juice au kinywaji chochote kile na ukafurahia.

Mahitaji

 • Unga wa ngano kilo 1
 • Amira vijiko 2 vya chai
 • Sukari vikombe viwili vya kahawa
 • Vanila ya unga nusu kijiko cha chai
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Nazi 1 tui zito
 • Mafuta lita 2

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chemsha mafuta mpaka yachemke, weka unga kwenye bakuli au sufulia.
 • Weka chumvi, amira changanya. Chota mafuta vikombe viwili vya kahawa weka kwenye unga.
 • Changanya vizuri na mwiko ( tumia mwiko sababu mafuta ni ya moto). Endelea kuchanganya na mikono mpaka unga uwe mlaini kabisa.
 • Uchanganyikane na mafuta vizuri, chukua tui weka sukari na vanila. Tui liwe la uvuguvugu, koroga mpaka sukari iyeyuke.
 • Weka kwenye unga, endelea kukanda. Kanda mpaka uone ukinyanyua unga kwa vidole, unanyanyuka wote haubaki kwenye sufuria.
 • Mwagia mafuta ya uvuguvugu juu ya unga uliokanda huku ukiendelea kukanda mpaka mafuta yasionekane kwenye unga.
 • Funika kwa dakika 5 uumuke,kisha anza kusukuma na kukata.Kata staili unayopenda.
 • Bandika mafuta jikoni. Yakipata moto weka maandazi yakigeuka rangi na kua kahawia geuza upande wa pili.
 • Ukiona yameiva epua. Tayari kwa kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Meat loaf
dakika 60
Walaji: 4

Mapishi ya nundu
dakika 15
Walaji: 3

Kuku wa kuoka
dakika 120
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.