Macaroni ya cheese

Chakula hiki ni kizuri sana, kinafaa kuliwa wakati wowote na kinywaji chochote. Na mkafurahi na familia

Mahitaji

 • Butter vijiko 2 vya chakula
 • Kitunguu maji 1
 • Maziwa vikombe 2
 • Macaroni mfuko 1
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai
 • Njegere robo kilo
 • Mustard kavu nusu kijiko cha chai
 • Curry powder kijiko 1 cha chakula
 • Garam masala nusu kijiko cha chai
 • Paprika kijiko 1 cha chakula
 • Tangawizi ya unga nusu kijiko cha chai
 • Kitunguu saumu nusu kijiko cha chai
 • Nyanya 2
 • Giligiliani nusu kijiko cha chai
 • unga (sweet corn) vijiko 2 vya chakula
 • Cheddar cheese vikombe viwili 2
 • Cumin nusu kijiko chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chemsha maji. Yakichemka weka macaroni na chumvi. Yakiiva chuja maji kisha weka macaroni pembeni.
 • Weka sufuria jikoni, weka butter. Weka kitunguu maji koroga kwa dakika 2.
 • Weka unga, koroga kwa dakika 1, weka tangawizi na kitunguu saumu koroga kiasi.
 • Weka nyanya, ache hadi iive vizuri kisha weka curry powder, garam masala na paprika. Koroga vizuri mchanganyiko.
 • Weka cumin, giligilian acha dakika 3 kisha weka chumvi kidogo. Koroga vizuri ili chumvi ichanganyikane.
 • Weka maziwa na mustard kwenye chombo bandika jikoni, koroga mpaka iwe nzito. Weka huo mchanganyiko kwenye viungo kisha koroga vizuri kwa dakika 2 alafu epua.
 • Ongeza cheese kwenye mchanganyiko wa maziwa.
 • Changanya macaroni, njegere na mchanganyiko wenye cheese. Koroga vizuri na hakikisha vimechanganyikana vizuri kabisa.
 • Mwagia pilipili manga kwa juu kisha weka mchanganyiko kwenye oven kwa dakika 20.
 • Epua na ujirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Viazi vya mboga mboga
dakika 18
Walaji: 2

Salad ya mahindi na samaki
dakika 0
Walaji: 2

Mkate wa kiwavi wenye kuku
dakika 40
Walaji: 6

Toa maoni yakoMinah
22:45, Fri 14 Nov 2014
Asante kwa hili pishi ni tamu sana
Dadia Msindai
01:47, Mon 17 Nov 2014
@Minah, Karibu sana. Ni kweli, hili pishi ni tamu haswa. Tunashukuru kwa feedback.
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.