Macaroni matamu yenye njegere

Macaroni ni chakula cha haraka, rahisi na bora kwa afya yako. Mchanganyiko wa nyanya, viungo na njegere kwenye macaroni unakuongezea ubora zaidi kwa kukupa virutubisho zaidi. Ni chakula unachoweza kuandaa kwa muda mfupi na kula pamoja na familia.

Mahitaji

 • Makaroni nusu packet
 • Nyanya 4 zilizoiva vizuri
 • Nyanya ya kopo (tomato paste)
 • Vitungui maji 2
 • Kitunguu saumu 1
 • Pilipili hoho 1
 • Soy sauce kijiko kidogo cha chai
 • Chumvi kiasi
 • Giligilani kijiko 1 cha chakula
 • Gharam masala robo kijiko cha chai
 • Curry powder kijiko 1 cha chai
 • Tangawizi nusu kijiko kidogo
 • Nazi 1 iliyokomaa
 • Njegere glass 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongeza au kupunguza viungo kutokana na upendeleo wako.

 • Kwenye sufuria, weka macaroni, maji na chumvi. Bandika jikoni, acha yaive kwa muda elekezi. Yakiiva, epua. Chuja maji kwenye macaroni – unaweza kutumia chujio au kitu kingine ulichonacho.
 • Andaa viungo. Menya nyanya,vitunguu maji 2, pilipili hoho, kitunguu saumu na nazi. Kata vizuri na hifadhi pembeni. Chemsha njegere ila zisiive sana.
 • Chuja tui zito la nazi. Hifadhi pembeni. Weka mafuta kwenye sufuria, acha yapate moto vizuri. Weka kitunguu maji. Pika kwa dakika 1 huku unakoroga. Weka kitunguu saumu, curry powder, tangawizi, giligilani ya unga na gharam masala. Koroga vizuri kisha weka nyanya. Koroga vizuri kisha acha ziive hadi zitengane na mafuta. Weka nyanya ya kopo (tomato paste) kiasi, koroga.
 • Weka njegere, koroga. Weka soy sauce na tui la nazi pamoja na chumvi kiasi. Weka makaroni kwenye sufuria. Changanya na sauce ya nyanya na njegere. Weka pilipili hoho, koroga na acha ziive kiasi, ili harufu iwe tamu na nzuri. Geuza mara kwa mara kisha acha chakula kichemke kidogo.
 • Epua chakula na jirambe.

misosi-njegere-macaroni


MAPISHI YAPENDWAYO

Dagaa wa kuunga na nazi
dakika 18
Walaji: 2

Roast ya maini
dakika 30
Walaji: 2

Kebab za nyama
dakika 15
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.