Macaroni ya bilinganya na nazi

Macaroni yana njia tofauti za kuandaa. Haya ni mojawapo ya mapishi ya kukupa macaroni matamu na yenye mvuto wa kumfanya mlaji afurahie chakula. Ni rahisi na haraka, hivyo ni chakula kizuri, chenye afya na bora kuandaa kama huna muda wa mwingi wa kukaa jikoni.

Mahitaji

 • Makaroni ½ packet, pima kutokana na mahitaji yako
 • Nyanya 4 zilizoiva vizuri
 • Nyanya ya kopo (tomato paste) vijiko 3 vikubwa
 • Vitunguu maji 2
 • Kitunguu saumu 1
 • Pilipili hoho 1
 • Soy sauce kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Giligilani kijiko 1 kikubwa
 • Gharam masala ¼ kijiko kidogo
 • Curry powder kijiko 1 kidogo
 • Tangawizi ½ kijiko kidogo
 • Nazi 1 iliyokomaa
 • Njegere glass 1
 • Bilinganya 1, kate vipande virefu na vyembamba
 • Italian seasoning kijiko 1 kidogo
 • Pilipili ndefu 2 kata vipande vidogo vidogo
 • Cayenne pepper kijiko 1 kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongeza viungo unavyopendelea ili kukifanya chakula kiwe kitamu. Ila kama unakula na watoto, hakikisha unapunguza uwingi wa pilipili, maana watoto wanaweza wasihimili ukali wake.

 • Andaa viungo – menya nyanya,vitunguu maji 2, pilipili hoho na kitunguu saumu. Kata vipande vidogo, hifadhi pembeni. Kamua tui zito la nazi, hifadhi pembeni.
 • Andaa njegere, zichemshe. Ila zisiive sana, epua na weka pembeni.
 • Kwenye sufuria, weka maji na chumvi, acha yachemke. Weka macaroni, pika kwa dakika 7 hadi 8 (fuata muda elekezi kwenye packet ya macaroni) kisha epua. Chuja maji, hifadhi pembeni.

Ni vizuri ukipika macaroni dakika 1 au 2 chini ya muda elekezi kwenye packet, hii itafanya macaroni yaive vizuri yakichanganywa na sauce na wakati wa kumalizia kupika.

 • Weka mafuta ya kula kwenye sufuria, bandika jikoni. Acha mafuta yapate moto vizuri kisha weka kitunguu maji. Hakikisha moto ni mkali ili mboga ziive vizuri bila kuchuja maji. Pika kwa dakika 2 huku unakoroga. Weka kitunguu saumu, curry powder, tangawizi, pilipili ndefu, giligilani ya unga, italian season na gharam masala. Koroga vizuri kisha weka nyanya. Koroga vizuri kisha acha ziive hadi zitengane na mafuta. Weka nyanya ya kopo (tomato paste) na bilinganya, koroga pamoja.
 • Weka njegere, koroga pamoja. Weka soy sauce pamoja na chumvi kiasi. Weka macaroni kwenye sufuria. Changanya na sauce ya nyanya na njegere. Weka pilipili hoho, koroga na acha ziive kiasi, ili harufu iwe tamu na nzuri. Weka tui la nazi. Geuza mara kwa mara kisha acha chakula kichemke kidogo. Nyunyizia cayenne pepper na pilipili manga ichanganye na chakula kisha epua.
 • Chakula kitakuwa tayari. Ili upate ladha zaidi, kula chakula hiki kikiwa bado cha moto.

macaroni-misosi-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Salad ya samaki
dakika 15
Walaji: 1

Mkate wa ndizi na mayai
dakika 75
Walaji: 16

Tambi na mayai
dakika 10
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.