Maharage ya nazi na karanga

Maisha ni kujaribu. Na mie siachi kujaribu mapishi. Hapa nachanganya maharage na viungo viwili murua ili kuyapa ladha tofauti na ya kipekee. Nilishazoea kula maharage yanayopikwa bila nyanya wala vikorombwezo tofauti, lakini leo hii napenda zaidi maharage yenye nyanya, maziwa, nazi na juu ya yote, nimeweka karanga. Uhondo wa mboga hii hauna kifani.

Mahitaji

 • Maharage 1/2 kilo
 • Nazi 1/2 kifuu
 • Karanga zilizosagwa au peanut butter vijiko 2 vikubwa
 • Bakuli ya plastiki
 • Chumvi
 • Nyanya
 • Karoti
 • Pilipili hoho
 • Kitunguu
 • Mchuzi wa kuku (supu baada ya kuchemsha kuku)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Recipe by Isatou Keita

 • Andaa maharage kwa kuyaosha na kisha bandika jikoni. Weka moto vizuri ili yapate kuiva. Maharage huchukua muda, hivyo ni vizuri kuangalia kila mara na kuongea maji ikiwezekana (kutokana na ugumu wa mharage unaweza kuongeza maji angalau mara 1. Maharage yaliyoiva hupasuka na kuvimba na kufanya maji yake kubadilika rangi)
 • Andaa viungo – osha na kisha kata kwenye vipande vidogo – kitunguu maji, nyanya, pilipili hoho na karoti. Tenga kwenye chombo pembeni.
 • Andaa tui la nazi – vunja nazi, kuna na kisha kamua tui zito. (Au kama utapata nazi ya dukani ni vizuri pia)
 • Maharage yakishaiva, ipua na kisha bandika sufuria nyingine jikoni, weka mafuta. Subiria yapate moto.
 • Weka kitunguu na koroga hadi kiive kwa kubadilika rangi, angalia kisiungue.
 • Weka nyanya, koroga na kisha funika ili zipate kuiva vizuri. Ponda nyanya ili kupata roho nzuri na mchuzi mzito.
 • Weka pilipili hoho, koroga kiasi acha kwa dakika 5 zichemke.
 • Weka maharage kwenye rojo huku unakoroga kidogo. Funika ili mchanganyiko uchemke.
 • Weka supu ya kuku, mimina huku ukiwa unakoroga ili ichanganyike vizuri.
 • Weka tui la nazi, koroga ili lichanganyike. Usiache kukoroga hadi lianze kuchemka. Hii inasaidia tui kutokatika na kupata mchuzi laini zaidi.
 • Andaa karanga za kusaga au peanut butter kwa kuweka vijiko 3 ya mezani kwenye bakuli ya plastiki. Ongeza maji vuguvugu kidogo sana (kama robo kikombe). Saga karanga, koroga au finyanga kwa mkono ili kuwa uji laini wa maji. Ni muhimu ziwe zimepondeka vizuri ili ziweze kuchanganyika kirahisi na mchuzi, lakini angalia maji yasiwe mengi sana.
 • Weka karanga kwenye mchuzi, koroga ili upate mchanganyiko vizuri kisha funika ili vipate kuiva.
 • Unaweza kuongeza pilipili manga kama utapenda.
 • Unaweza kuchemsha pilipili nzima (kuwa makini usiipasue) ili kuyapa maharage harufu nzuri.
 • Maharage haya huweza kuliwa kwa vitu tofauti, mie hupendelea zaidi na wali wa nazi.

Jirambe na uhondo wa maharage. Washirikishe uwapendao kwa kuwapa link hii ya mapishi.


MAPISHI YAPENDWAYO

Pilau la basmati
dakika 35
Walaji: 4

Beef Masala
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.