Majani ya kitunguu (Leek) na ugali

Mboga hii ni rahisi kuandaa. Mie binafsi nilifurahi kula yenyewe tu bila kuongeza mchuzi, sababu nilikula na ugali. Unaweza pia kula kama mboga ya ziada na chakula na pia ikanoga.

Mahitaji

  • Jani ya kitunguu 1 (Linakuwa shina zima)
  • Karoti 1
  • Mafuta ya kula kijiko 1 kikubwa
  • Kitunguu saumu 1
  • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
  • Sauce ya kuku (Hii si lazima, mie nimetumia mchuzi mix)
  • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kitu muhimu kabisa wakati unaandaa hii mboga hakikisha umekata vipande vidogo ili iive haraka na vizuri. Vikiwa vipande vikubwa sana huwa inachelewa kuiva. Hii itakusaidia kuokoa virutubisho vilivyomo kwenye mboga na muda wako pia.

misosi-majani-kitunguu2

  • Menya kisha kata karoti. Menya kisha ponda kitunguu saumu. Kata kitunguu cha majani vizuri, osha na kisha weka kwenye chombo safi.
  • Weka mafuta kwenye kikaango, bandika jikoni. Hakikisha moto ni mkali sana ili mboga iive vizuri. Mafuta yakipata moto weka kitunguu saumu. Koroga kiasi. Weka majani ya kitunguu, koroga vizuri. Funika kwa takribani dakika 3 hadi 5. Funua, koroga kiasi. Ongeza karoti kwenye kikaango, koroga vizuri. Funika acha viive kwa pamoja kwa dakika 3. Weka pilipili manga kisha ongeza sauce (kama unatumia). Koroga vizuri kisha funika acha viive. Ikishaiva bandua jikoni, hifadhi pembeni.

Mboga ikipikwa kwenye moto mdogo (hafifu) huwa inachuja sana maji matokeo yake haiivi vizuri au inakosa utamu, hivyo hakikisha moto ni mkali ili mboga iive vizuri. Kuwa makini usiunguze.

  • Songa ugali unaokutosha. Kisha tenga ujirambe na chakula chako kitamu.

ugali-majani-kitunguu


MAPISHI YAPENDWAYO

Sambusa za nyama
dakika 15
Walaji: 10

Macaroni ya cheese
dakika 20
Walaji: 3

Peanut butter cookies
dakika 10
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.