Mapishi 3 ya Butternut squash kwa watoto

Aina tatu za mapishi unayoweza kuandaa na butternut squash. Ni rahisi kuandaa na chakula ni kizuri kwa afya pia.

Mahitaji

Mahitaji yanatofautiana na pishi lipi unalotaka kuandaa:

 • Butternut squash
 • Spinach
 • Maziwa
 • Maji
 • Pilipili manga
 • Mafuta ya kula (Nimetumia olive oil)
 • Kitunguu saumu
 • Kitunguu maji

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Haya ni mapishi matatu kati ya mengi unayoweza kuandaa butternut squash. Mapishi haya tuliyoelezea hapa ni maalum kwa mtoto mdogo, kuanzia takribani miezi 6, ndio maana tunashauri chakula kisagwe. Butternut squash ni tunda jamii ya boga na lina virutubisho zaidi ya boga. Ni nzuri zaidi hasa kwa watoto wanaohitaji vyakula bora ili kuweza kukua vizuri.

PISHI 1:

 • Menya butternut, kata vipande vidogo weka pembeni.
 • Weka butter kwenye sufuria, ongeza maji au maziwa kidogo, pika hadi liive.
 • Likiiva, toa weka kwenye blender. Saga, subiri kipoe mpe mtoto.

PISHI 2:

 • Katakata butternut na spinach kwenye vipande vidogo.
 • Bandika sufuria jikoni, weka olive oil. Yakipata moto weka butternut, koroga kama dakika 5, weka spinach. Kaanga kama dakika 3. Weka maji, maziwa au supu kidogo. Acha vichemke kidogo kisha epua.
 • Weka kwenye blender, saga na mpe mtoto.

PISHI 3:

 • Washa oven, weka nyuzi joto 350°F(180°C), andaa chombo cha kuokea kwa kukipaka mafuta.
 • Kata butternut kwa juu kama picha inavyoonyesha, toa mbegu na yale makamba kamba.
 • Weka kwenye chombo cha kuokea, paka mafuta ya olive oil ndani ya butternut, nyunyizia chumvi na pilipili manga kiasi ili liwe na ladha tamu. Weka kwenye oven. Kama anakula mtu mzima unaweza kuongeza viungo unavyotaka - mfano thyme, parsley n.k
 • Acha liive mpaka ngozi ya nje iwe laini. Toa weka pembeni.
 • Kata kuku vipande vidogo. Weka mafuta kwenye kikaangio jikoni, acha yapate moto. Weka kuku, kaanga mpaka aanze kubadilika rangi. 
 • Weka kitunguu maji,  saumu, na spinach. Koroga dakika 3. Epua, jaza kwenye butternut kisha weka kwenye oven kama dakika 20. Toa, acha kipoe.
 • Mpe mtoto ajirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Butter chicken
dakika 45
Walaji: 4

Garlic chicken
dakika 60
Walaji: 4

Spicy grilled prawns
dakika 35
Walaji: 3

Lemon mustard chicken
dakika 45
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.