Mapishi ya ndegu kwa watoto

Chakula hiki ni kitamu, utafanya mtoto afurahi na ale sana mana atapata hamu ya kula zaidi. Na pia atapata virutubisho muhimu kwa ujenzi wa mwili na afya yake.

Mahitaji

 • Ndegu robo kilo
 • Kitunguu saumu punje 3
 • Limao robo kipande
 • Olive robo kijiko cha chai
 • Binzari nyembamba kiasi
 • Paprika kiasi
 • Chumvi kiasi ( weka kuanzia mtoto wa mwaka na kuendelea)
 • Tahini kikombe 1   (  Tahini ni mchanganyiko wa ufuta na olive, zikaange mbegu za ufuta huku ukizigeuza geuza mpaka ziwe za brown, weka kwenye blender weka na olive oil kisha saga uzito unaotaka).        

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Osha dengu, chemsha kwa dakika 60 mpaka ziwe laini na maganda yaanze kutoka.
 • Dengu zikiwa bado jikoni, chukua blender weka tahini, maji ya limao, kitunguu saumu, olive oil, binzari nyembamba na paprika, saga zilainike kabisa.
 • Weka pembeni usitoe kwenye jagi la kusagia, dengu toa maganda kisha weka kwenye blender, saga mpaka zilainike kabisa.
 • Zikiwa nzito sana, ongeza maji endelea kusaga. Mpe mtoto ajirambe.
 • Chakula hiki anza kumpa mtoto wa miezi 9 (usiweke chumvi ) na kuendelea.

MAPISHI YAPENDWAYO

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.