Mapishi ya nundu

Nundu ni aina ya nyama ambayo hupatikana kwenye ng'ombe. Nyama hii ina mafuta sana unaweza kuipika yenyewe au ukachanganganya na chakula kingine.

Mahitaji

 • Nyama lakini iwe nundu
 • Tangawizi ya unga
 • Vitunguu saumu
 • mdalasini
 • Chumvi
 • Soy sauce
 • Currypowder
 • Pilipilimanga
 • Maji
 • Vitunguu maji visage viwe uji
 • Ndimu

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Osha nyama vizuri, ikamulie ndimu ya kutosha. Weka tangawizi kiasi na vitunguu saumu kisha bandika jikoni.
 • Hakikisha nyama imeiva vizuri sana, ibaki na mchuzi kidogo. 
 • Weka vitunguu maji ulivyovisaga kisha funika. Iache iendelee kuchemka vitunguu viive. 
 • Hakikisha mpaka maji yanakauka, hiyo nyama inamafuta sana. 
 • Itaanza kujikaanga hapo weka mdalasini na curry powder koroga mpaka uone nyama inabadilika rangi kua ya kahawia, usiache kukoroga mana itashika chini.
 • Ongeza soy sauce au oyster sauce au sause yoyote uliyonayo. Koroga ichanganyikane vizuri na nyama yako.
 • Ongeza tangawizi na pilipili manga, unaweza kutumia hata pilipili mbuzi.
 • Koroga mpaka yale maji ya soy sauce yakauke, kamulia ndimu koroga kwa dakika 5 msosi wako utakua tayari kijiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa mchuzi
dakika 25
Walaji: 4

Broccoli ya bamia
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.